Na Avelina Musa - Dodoma.
Hayo yamesemwa Leo August mosi na Abdulrahman Msham, Mkurugenzi Msaidizi huduma za Sheria kwa Umma kutoka wizara ya Katiba na Sheria katika maonesho ya siku kuu ya wakulima Nane nane(8)ambayo kitaifa yanafanyika Jijini Dodoma.
Amesema wizara hii imepewa idhini ya kusimamia masuala ya haki,Sheria na katiba ambapo watakapofika katika Banda hilo watapata elimu ya Sheria zote za nchi na watapata huduma mbalimbali.
Abduramani amesema kero nyingi wanazozipokea mara kwa mara ni migogoro ya ardhi na migogoro ya mirathi pamoja na migogoro ya ndoa na talaka hasa katika mgawanyo wa mali baada ya ndoa na talaka.
"Sisi tupo hapa katika maonesho haya ambapo tunatoa huduma ya kutatua migogoro na elimu ya utatuzi wa migogoro pamoja na elimu ya haki za binadamu."Amesema Abduraham.
"Na migogoro yote hii inatokana na watanzania kukosa elimu sahihi ya sheria ambapo ukosefu wa elimu ya Sheria inawafanya wanaingia katika migogoro isiyo ya lazima kama kutokuandika wosia."Amesema.
Maonesho ya sikukuu ya wakulima nane nane (88)yanafanyika kitaifa Jijini Dodoma kuanzia Leo August mosi Hadi August 8 mwaka huu ambayo yanaongozwa na kauli mbiu isemayo "Chagua viongozi Bora kwa maendeleo Endelevu ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi 2025".