WAFANYABIASHARA KARIAKOO KUWENI MABALOZI WA AMANI - DKT. JAFO

MUUNGANO   MEDIA
0

 


Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt. Selemani Jafo amewataka wafanyabiashara wa Soko la kimataifa la Kariakoo kuwa mabalozi wa amani ili biashara zifanyike kwa utulivu na usalama kipindi hiki nchi ikielekea kwenye Uchaguzi Mkuu, kauli aliyoitoa leo Agosti 15 ,2025 wakati akifungua tamasha la Gulio la Kariakoo, Dar es Salaam.



Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt. Selemani Jafo akiwa kwenye picha ya pamoja na wakuu wa taasisi za umma zinazohusika na usimamizi na uratibu wa wafanyabiashara nchini leo wakati wa uzinduzi wa tamasha la Gulio la Kariakoo jijini Dar es Salaam leo Agosti 15,2025.


Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato (TRA) Bw. Yusuph Mwenda amesema wataendelea kusikiliza na kutatua kero za wafanyabiashara wa Kariakoo ili walipe kodi kwa uaminifu .


 Mratibu wa tamasha la Gulio la Kariakoo (Kariakoo Festival) George Lupenza amesema tamasha hilo litafanyika ndani ya saa 72 kuanzia leo na lengo ikiwa ni kutoa fursa kwa wafanyabiashara kupata masoko ya bidhaa zao ndani na nje ya nchi.

Na Mwandishi Wetu- Dar es salaam 

Wafanyabiashara wa Soko la Kariakoo wametakiwa kuwa mabalozi wa kuhakikisha nchi inaendelea kuwa na amani kipindi chote cha kuelekea Uchaguzi Mkuu ili shughuli za biashara zifanyike kwa usalama huku wakilipa kodi kwa uaminifu.
Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt. Selemani Jafo wakati wa hotuba yake ya ufunguzi wa tamasha la Gulio la Kariakoo (Kariakoo Festival) leo (15 Agosti 2025) Dar es Salaam lenye lengo la kutangaza fursa za biashara na masoko yaliyopo nchini.
Tarehe 29 Oktoba mwaka huu tutakuwa na Uchaguzi Mkuu, niwaalike wafanyabiashara wa Kariakoo kuwa mabalozi wa amani ili shughuli za kibiashara katika eneo lote la Kariakoo na Tanzania kwa ujumla zifanyike kwa amani na utulivu.
Naye Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) Yusuph Mwenda alisisitiza kuwa iko tayari kuendelea kuwasikiliza wafanyabiashara na kutatua kero zao ili walipe kodi kwa mujibu wa Sheria.
Mwenda aliongeza kuwataka wafanyabiashara kote nchini kuendelea kulipa kodi kwa uaminifu ili Serikali ipate mapato ya kutekeleza miradi ya maendeleo.
Kwa upande wake Meneja Mkuu wa Shirika la Masoko ya Kariakoo CPA Ashraph Abdulkarim alieleza kuwa tamasha hilo ni fursa nzuri kwa wadau wa Soko la Kariakoo kuwafikia wateja ndani na nje ya nchi.
CPA Abdulkarim aliongeza kusema, Shirika lipo kwenye maandalizi ya mwisho kuelekea kurejesha wafanyabiashara ndani ya Soko baada ya Serikali kukamilisha ujenzi na ukarabati wa soko ambapo amemshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha Bilioni 28.


Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)