NGOs ZATAKIWA KUWA NA NJIA MBADALA KUENDELEZA MIRADI KWA KUTUMIA RASILIMALI : DKT. JINGU

MUUNGANO   MEDIA
0

 




Na Avelina Musa -  Dodoma 

Mashirika Yasiyo ya Kiserikali yametakiwa  kujitafakari vizuri ili kuhakikisha yanakuwa na njia mbadala kuendeleza huduma na miradi kwa kutumia rasilimali zinazopatikana katika maeneo yao. 


Hayo yamesemwa leo Agosti 12, 2025 na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt John Jingu wakati anazungumza katika Kongamano la Mashirika Yasiyo ya Kiserikali linaloendelea kwa siku ya pili katika Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma. 




Amesema ili kazi za mashirika ziendelee kuwa nzuri na endelevu inabidi kuwa na rasilimali fedha ambazo zinapatikana kwa njia ambazo zinawezekana ndani ya nchi.

Dkt. Jingu amesema Mashirika hayo yanawajibu wa kuleta mabadiliko ya kiuchumi, kifikra na maendeleo katika jamii kupita utekelezaji wa miradi yao mbalimbali. 

“Mashirika Yasiyo Ya Kiserikali, yamesajiliwa kisheria kwa lengo la kutoa huduma na elimu katika nyanja tofauti kwa jamii hivyo mtambue kwamba ajenda ya maendeleo endelevu katika Taifa ni pamoja na kuwa mawakala wa mabadiliko chanya katika jamii” amesema Dkt Jingu. 


Aidha amesema kwamba Mashirika yanapaswa kutekeleza miradi ya uzalishaji ambayo ni endelevu na kuondoa utegemezi kutoka kwa wafadhili, kwa sababu kwa sasa Sera za nchi za Ulaya na Marekani zimebadilika.


Kongamano hilo la siku tatu litarajiwa kuhitimishwa kesho ambapo Makamu wa Rais, Dk.Philip Mpango anatarajiwa kuwa mgeni rasmi.






Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)