MHE. SENYAMULE AIPONGEZA EWURA CCC KWA HUDUMA NZURI

MUUNGANO   MEDIA
0

 


Na Avelina Musa - Dodoma.



Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,Mhe. Rosemary Senyamule, ameipongeza  Baraza la Ushauri la watumiaji wa huduma za nishati na maji (EWURA CCC)kwa kutoa huduma nzuri tangu kuanzishwa kwake huku akiishauri kuimarisha elimu kwa wananchi ikiwa ni pamoja na kufika maeneo ya vijijini ili kuongeza uelewa wa huduma hizo muhimu.


Mhe.Senyamule amesema hayo leo Agosti 5, 2025 alipotembelea banda la Baraza hilo katika Maonesho ya Wakulima Nanenane yanayoendelea katika viwanja vya Nzuguni jijini Dodoma.

"Hongereni sana mmekuwa na huduma nzuri lakini sasa muende na vijijini ili hata wananchi wa vijijini wapate elimu hii muhimu."Amesema Mhe,Senyamule.

Kwa upande wake Afisa uelimishaji na uhamasishaji kutoka baraza hilo Bwn.Ligiko Lugiko amesema katika kusimamia matumizi ya nishati  safi baraza inasimamia mkakati wa mwaka 2024 mpaka 2034 kwaajili ya matumizi ya nishati safi.

Amesema Matumizi ya nishati safi ya kupikia ni kitu halisi na ni kitu kinachowezekana sio vitu vya kufikirika,ambapo watanzania wanaweza kupika kwa umeme, gesi na huduma zote hizi zinapatikana na bei zinafikika kwa watanzania walio wengi.

"Niiombe Serikali inapohamasisha matumizi ya nishati safi watumiaji wahamasike kuhamia huko kwasababu ipo faida kubwa ya kiafya wanaipata ikiwemo kujiepusha na maradhi yatokanayo na matumizi ya nishati chafu."Amesema.


Lugiko amesema banda la EWURA CCC limekuwa likitoa elimu kwa vikundi vya wanawake, vijana na wakulima wadogo,kuhusu namna huduma bora za nishati na maji zinavyoweza kuongeza thamani ya mazao kwa kutumia kilimo cha kisasa na gesi asilia katika usindikaji wa mazao

Hata hivyo  baadhi ya wananchi waliofika katika Banda la Ewura CCC wamepongeza kwa elimu inayotolewa na baraza hilo kwani imeweza kuwafungua kifikra kutokana na yale waliyojifunza ikiwemo namna ya kuwasilisha malalamiko yao yanayohusiana na umeme, maji, gesi pamoja na petroli.

“Tunawapongeza EWURA CCC kwa elimu waliotupatia siku ya leo kwani hatukujua kama kuna watu wanaoweza kututetea kutokana na huduma tunayopatiwa, kwasababu unakuta muda mwingine tunapata changamoto mbalimbali lakini hatuna sehemu ya kuzupeleka,”wamesema.




Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)