Na Avelina Musa - Dodoma
Hayo yamesemwa na Wakili wa serikali Mkuu kutoka Bank kuu ya Tanzania (BOT) Bwn.Stanford Mbengane wakati akizungumza na waandishi wa habari katika maonesho ya wakulima nane nane 88)yanayoendelea katika viwanja vya Nzuguni Jijini Dodoma.
Amesema BOT wapo katika Maonesho ya nane nane kwa ajili ya kutoa elimu kwa wananchi kuhusu utakatishaji wa fedha haramu ambapo ni fedha iliyopatikana kwa njia isiyo halali.
Mbengane amesema Bank kuu inajukumu la kuhakikisha fedha zinazoingia katika mifumo ya Tanzania ni fedha halali ili kulinda uchumi wa watanzania kuwa salama.
Amesema wapo wanaouza dawa za kulevya na kufanya biashara haramu ya binadamu na kuziwekeza kwenye aseti zao ambapo ni vitendo vya uvunjifu wa Sheria.
"Ili kulinda uchumi wetu taasisi zote za Bank na watoa huduma za fedha wanatakiwa kupitia mara kwa mara taarifa na mienendo ya miamala ya wateja wao ili kubaini vitendo vya utakatashaji fedha haramu."Amesema Mbengane.
Aidha Mbengane amesema mpaka sasa Tanzania imetolewa kwenye orodha za Nchi zenye Utakatishaji wa Fedha ambapo tayari imekidhi vigezo vya kimataifa.