DC SHEKIMWERI AIPONGEZA WIZARA YA KATIBA NA SHERIA.

MUUNGANO   MEDIA
0


 

Na Avelina Musa - Dodoma.

 Wizara ya Katiba na Sheria yapongezwa kwa kuendelea na utekelezaji wa kampeni ya msaada wa kisheria wa mama Samia legal Aid ambayo imesaidia  kupunguza migogoro mingi Nchini.


Hayo yamesemwa Leo Agosti 6.2025 na  Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini Mhe. Jabir   Shekimweri    alipotembelea banda la Wizara ya Katiba na Sheria na kuongeza kuwa utekelezaji wa Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia utasaidia kupunguza migogoro hususan ya ardhi ambayo bado ni mingi katika mkoa wa Dodoma.


“Nimefurahi sana kukuta banda la Wizara ya Katiba na Sheria linatoa huduma hii ya Msaada wa kisheria lakini pia inatoa elimu hivyo natoa wito kwa wananchi wote wafike hapa kupata elimu na huduma ya utatuzi wa migogoro, lakini pia kinamama mjitokeze kwa wingi kujifunza Masuala ya mirathi kwani nyie ndio wahanga wa masuala hayo”, amesema.



Amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi kwani wizara hiyo inashughulikia na kusikiliza kero, malalamiko na changamoto mbalimbali hivyo basi watumie fursa hiyo kupata ufumbuzi wa changamoto zinazowakabili kutoka kwa wataalamu wa kisheria.


Aidha Shekimweri amepongeza utoaji wa Elimu ya Haki na Utawala Bora inayotolewa kwani itawafaa wananchi katika kipindi hiki cha kuelekea katika uchaguzi Mkuu.


“Tunaelekea katika kipindi cha Uchaguzi Mkuu kwahiyo wananchi wanaofika katika banda hili wananufaika na elimu hii itakayowasaidia kutambua wajibu na haki zao ili waweze kushiriki kikamilifu katika uchaguzi huo,” amesisitiza Shekimweri.



Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)