Na Avelina Musa - Dodoma.
Chuo cha Bank kuu (BOT Academy)yaendelea kutoa kozi 57 za muda mfupi kwa washiriki kutoka Tanzania na nje ya Tanzania na mafunzo ya muda mrefu katika kozi mbili.
Ambayo ni Ordinary Diploma in banking practice and supervision na Post graduate Diploma in Banking Managemant na kwa sasa dirisha lipo wazi kupitia website ya chuo ambayo ni www.academy@bot.go.tz
Hayo yamesemwa leo Jijini Dodoma na Mratibu wa Mafunzo Chuo cha Bank kuu CPA.Mukrim Ramadhani wakati akizungumza katika maonesho ya wakulima nane nane(88)yanayoendelea Nzuguni Jijini hapa.
Amesema wapo katika maonesho hayo ili kueleza majukumu ya chuo Cha bank kuu ambapo amesema chuo hicho kimeanzishwa mwaka 1991 Jijini Mwanza kwa lengo la kuwajengea uwezo wafanyakazi wake ili kuongeza tija katika utendaji wao lakini kwa sasa imetoa fursa kwa watanzania wote kupata mafunzo ya muda mfupi na muda mrefu
CPA.Mukrim amesema chuo hicho pia kinatoa certification programme, ambazo ni certified Currence management, microfinance certification programme, certified financial educator na certified credit analysis.
Aidha amesema Sifa za kujiunga kwa upande wa diploma ni principle pass Moja na subsidiary Moja ambayo ni E na S au certificate inayo endana na maswala ya fedha na upande wa postgraduate awe na degree yoyote kutoka katika chuo kinacho tambulika na serikali.
Mwisho.