WAPIGA KURA MILION 37.6 WAJIANDIKISHA KUPIGA KURA MWAKA 2025

MUUNGANO   MEDIA
0

 




Na Avelina Musa - Dodoma.



TUME huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) imesema  Wapiga Kura million  37,655,559 wamejiandikisha  kupiga kura katika Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani unaotarajiwa kufanyika October 29.2025.

 Ambapo Idadi hii ni sawa na ongezeko la asilimia 26.55 kutoka idadi ya 
wapiga kura million 29,754,699 waliokuwa kwenye Daftari, mwaka 2020.

Hayo yamesemwa Leo Jijini Dodoma na Mwenyekiti wa Tume huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) Mhe.Jaji  (Rufaa) Jacobs  Mwambegele,wakati wa  Uzinduzi wa Ratiba ya Uchaguzi wa Rais na wabunge katika Jamhuri ya Muungano na madiwani kwa Tanzania Bara mwaka 2025.

Mhe. Jaji Mwambegele  amesema kwa upande wa Zanzibar, Wapiga Kura 725,876 wapo katika Daftari la Wapiga Kura la ZEC na wapiga kura 278,751wameandikishwa na INEC kwa kuwa hawakuwa na sifa za kuandikishwa na ZEC.

"Katika idadi ya wapiga kura 37,655,559 waliopo katika Daftari, wapiga kura 
36,650,932 wapo Tanzania Bara na Wapiga Kura 1,004,627 wapo Tanzania 
Zanzibar."Amesema.


Aidha amesema jumla ya vituo 99,911vitatumika kupigia kura kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 
ambapo idadi hiyo ya vituo 99,911 ni sawa na ongezeko la asilimia 22.49 ya vituo vya kupigia kura.


Akizungumzia  Ratiba ya Uchaguzi  Mhe.Jaji Mwambegele amesema Agosti 09.2025 hadi Tarehe 27 Agosti, 2025 utoaji wa fomu za uteuzi kwa wagombea wa nafasi ya Rais na Makamu wa Rais  ambapo Agosti 27 2025 itakuwa siku ya uteuzi wa wagombea wa kiti cha rais na makamu rais, uteuzi wa wagombea ubunge na uteuzi wa wagombea udiwani.

Mhe.Jaji Mwambegele amesema kuanza kwa kampeni, Tanzania Bara itakuwa  kuanzia Agosti 28 hadi Oktoba 28, huku Tanzania Zanzibar kampeni zikiendeshwa kuanzia Agosti 28 hadi Oktoba 27, ili kupisha upigaji wa kura ya mapema.

Kwa Upande wake Katibu Mkuu wa chama cha NCCR Mageuzi Bi.Evelyn Munisi ameipongeza Tume kwa Utendaji wake mzuri na ameongeza kuwa hawana mashaka na Tume na wao wamejipanga kushiriki Uchaguzi Mkuu.

Hata hivyo Bi.Evelyn amewaasa watanzania kudumisha amani katika kipindi cha kampeni na wakati wa Uchaguzi ili Taifa liendelee kuwa na amani.






Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)