Na Avelina Musa - Dodoma.
KATIKA kuelekea maadhimisho ya Siku kuu ya Wakulima nanenane ambayo Kitaifa mwaka huu yanafanyika Mkoani Dodoma,Benki ya maendeleo ya Kilimo (TADB) imetoa million 400 kwa ajili ya kufadhili maonesho hayo kama sehemu ya shukrani yao kwa mafanikio makubwa waliyoyapata tangu kuanzishwa kwake.
Hayo yamesemwa leo Jijini Dodoma na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo,Bwn Michael Noel wakati akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusiana na maonyesho hayo ambayo yanatarajiwa kuzinduliwa Agosti Mosi Mwaka huu huku mgeni rasmi akitarajiwa kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Amesema utashi wa kisiasa wa Mhe,Rais Dkt.Samia umefanya bank ya TADB kuwa benk kubwa kwa kuiwezesha kufanya vizuri katika utendaji wake kwa kuongeza bajeti.
"Tumeamua kuwa wadhamini kwa sababu sisi ndo wenye dhamana ya kusimamia kilimo na Katika siku hizi nane za maonesho tumejipanga kuhudumia wananchi.
Amesema maadhimisho ya mwaka huu yanaambatana na maadhimisho ya miaka kumi (10)ya benk ya maendeleo ya kilimo TADB ambapo benk hii imepata mafanikio makubwa tangu kuanzishwa kwake.
Aidha amesema Bank imetoa Mikopo ya riba nafuu kwa Wakulima yenye jumla ya Shilingi Trilioni1.2 katika kipindi cha miaka minne kwa lengo la kuwainua wakulima.
Awali Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo,Bw.Gerald Mweli amesema kuwa Maonyesho ya Mwaka huu yameboreshwa ambapo pia ni kitivo cha kutoa Elimu kwa wakulima na wananchi.
Maonyesho ya nanenane Kitaifa kwa mwaka huu 2025 yanadhaminiwa na benki ya maendeleo ya kilimo (TADB) kama mdhamini mkuu ambayo yatafanyika kuanzia Agosti mosi hadi agosti 8 katika viwanja vya Nzuguni Jijini Dodoma.


