Rai hiyo ilitolewa Julai 06, 2025 na Polisi Kata wa Mwakakati Mkaguzi wa Polisi Robert Kasunga alipokuwa anatoa elimu juu ya madhara ya kuwaita watoto majina ya wanyama, alisema kuwa inaonyesha kuwa kundi kubwa la watoto uathirika na kutaniwa majina hayo hasa wakiwa mashuleni, mitaani, na hata majumbani, jambo linalowasababishia madhara ya kisaikolojia na kupunguza hali yao ya kujiamini na kutotimiza malengo ya masomo yao.
Mkaguzi Kasunga, aliwataka wazazi, walezi na jamii kwa ujumla kuacha tabia ya kuwadhalilisha watoto kwa maneno au matendo kwani alisema watoto wana haki ya kulindwa, kuheshimiwa, na kulelewa katika mazingira salama kwani huo ni moja ya aina ya ukatili wa kijinsia na kihisia unaoweza kuwa na athari kubwa katika maisha ya mtoto katika ukuaji wa maisha yake.
Pamoja na hilo, Mkaguzi Kasunga, alitoa tahadhari kwa yeyote atakayebainika kujihusisha na vitendo vya aina hiyo atachukuliwa hatua kali kwa mujibu wa sheria, ikiwa ni pamoja na Sheria ya Mtoto Na. 21 ya mwaka 2009 inayolinda haki na ustawi wa mtoto.
Mwisho, Mkaguzi Kasunga alihitimisha elimu hiyo kwa waumini hao kwa kusema MSIWAITE WATOTO MAJINA YA WANYAMA WAHESHIMU, WAWAPE UPENDO, WAJENGEKE NA WAWE FAIDA NA HAZINA YA KESHO KWA TAIFA LETU. na aliwataka waumini hao kutoa taarifa au malalamiko ya aina hiyo kwa Jeshi la Polisi Mkoa wa Songwe au kwenye Dawati la Jinsia na Watoto katika kituo cha Polisi kilicho karibu ili ziweze kushughulikiwa kwa haraka.



