JESHI LA POLISI LAFANYA UKAGUZI MAGARI YA SHULE NA LATOA ELIMU YA USALAMA BARABARANI.

MUUNGANO   MEDIA
0

 Na Issa Mwadangala.


Katika kuhakikisha Mkoa wa Songwe unaendelea kuwa salama Jeshi la Polisi Mkoa wa Songwe linaendelea kudhibiti ajali zinazosababishwa na madereva wasio fuata sheria za usalama barabarani kwa kufanya ukaguzi wa magari ya shule na kutoa elimu juu ya madhara ya kuendesha magari mabovu na kutokuwa na leseni ya chombo husika.        
                                                       
Akiongea na wamiliki na walimu wa shule za Wilaya ya Mbozi Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Augustino Senga amesema kuwa leo Juni 23, 2025 amekutana na wamiliki, madereva na wasimamizi wa wawatoto wa shule Mkoani humo kwa lengo la kutoa elimu na ukaguzi wa vyombo vyao ili kubaini uimara na ubovu wa magari hayo kwa lengo la kuepuka ajali zinazoweza kuzuilika.

Kamanda Senga ameongeza kuwa “tumeona tuwaite wamiliki na madereva wa shule ili tukague vyombo vyenu vya moto kabla shule hazijafunguliwa na tumetoa muda maalum takilibani siku 14 na baada ya kipindi hicho kupita kwa wale wote ambao hawatokuwa wamekaguliwa watazuiliwa kutoa huduma na hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao”
 
Sambamba na hilo, Kamanda Senga alisema zoezi hilo litakuwa endelevu likiambatana na magari mengine ambayo ni ya abiria na yasiyo ya abiria ikiwa ni pamoja na yale yanayofanya usafirishaji usio rasmi ambao unafanyika mashambani katika kipindi hiki cha mavuno wakiwa wanabeba watu na kuwachanganya na mizigo kwa kutumia usafiri wa maguta kitendo ambacho ni kinyume na sheria za usalama barabaranina na kwa wale wote watakao bainika hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao ili iwe fundisho kwa watu madereva wengine wenye tabia kama hizo.

Vilevile Kamanda Senga alitoa wito kwa wamiliki na madereva shule kufika kwa wakati katika kikosi cha Usalama barabarani Mkoa kufanya ukaguzi wa magari yao na kupata elimu juu ya matumizi sahihi ya sheria za usalama barabarani ili kuendelea kutoa huduma katika hali ya salama na kuepuka ajali zinazoweza kuepukika.

Judith Kamwela ambaye ni msimamizi wa watoto kwenye magari ya shule ya msingi Oswe amebainisha faida ya ukaguzi wa magari hayo ikiwa kuepusha ajali za barabarani na kusaidia kubaini ubovu wa gari. Pia alitumia fursa hiyo kuliomba Jeshi la Poliai Mkoa wa Songwe kuendelea na zoezi hilo ili kusaidia usalama wa vyombo hivyo ikiwa ni pamoja na wanafunzi ambao wanawapa huduma ya usafirishaji huo pindi wanafunzi waendapo na warudipo shuleni.

Naye, Shukurani Kota ambae ni Mwalimu wa usimamizi wa magari shule ya God’s Bridge licha ya kupongeza Jeshi la Polisi amesema ukaguzi wa magari hayo ni juhudi madhubuti za kupunguza ajali na kuhakikisha usalama kwa wanafunzi wa shule pia ameona ni muhimu zoezi hilo liwe mara kwa mara ili kuendelea kupunguza ajali za barabarani.

Kwa upande wake, Koplo Said Mjaliwa ambaye ni Mkaguzi wa magari wa Polisi Mkoa wa Songwe amesema kuwa jumla ya magari ya shule 03 yamekaguliwa kati ya shule 12 na kukutwa magari 03 mabovu ambayo yanatakiwa kufanyiwa matengenezo, pia amewataka wamiliki wa shule zilizobaki kuleta mgari yao kabla ya tarehe 01 mwezi wa 07 mwaka 2025 ili kukwepa mkono wa sheria vilevile amewataka wamiliki wa shule na wasimamizi wa watoto kutokuzidisha wanafunzi katika magari hayo bali amewataka kupakia wanafunzi kutokana na uwezo wa gari husika ili kuepusha madhara makubwa pindi tatizo au ajali inapotokea.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA SONGWE SACP SENGA

WhatsApp Image 2025-06-23 at 16.29.58_88b58448.jpg

KAMANDA SENGA AKIONGEA NA WAMILIKI NA MADEREVYA WA MAGARI YA SHULE
WhatsApp Image 2025-06-23 at 16.29.58_a6fb559a.jpg

WhatsApp Image 2025-06-23 at 16.29.59_853e27f2.jpg
WhatsApp Image 2025-06-23 at 16.29.59_cf473255.jpg
WhatsApp Image 2025-06-23 at 16.30.00_2f31723a.jpg
WhatsApp Image 2025-06-23 at 16.30.00_a08c91dc.jpg
WhatsApp Image 2025-06-23 at 16.30.00_c545c748.jpg
WhatsApp Image 2025-06-23 at 16.30.01_d1b15923.jpg
WhatsApp Image 2025-06-23 at 16.30.01_11fd01e4.jpg
WhatsApp Image 2025-06-23 at 16.30.02_a7a2edca.jpg

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)