Maonyesho ya kilimo ya nanenane yanatarajiwa kufanyika kitaifa Mkoani Dodoma katika Viwanja vya Nzuguni huku Wadau mbalimbali wa Kilimo wakishauriwa kujisajili kwa Tovuti kuanzia Juni17 Mwisho wa usajili ni Julai16 Mwaka huu.
Waziri wa Kilimo,Hussein Bashe ameyasema hayo Juni13 Jijini Dodoma wakati akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusiana na maonyesho hayo.
Aidha Waziri Bashe amebainisha kuwa lengo la tovuti hiyo ni kurahisisha usajili wa Wadau wa Kilimo wa ndani na nje ya nchi katika kuwasilisha maombi ya huduma ya Mabanda kwaajili ya maonesho.
"Wizara ina hamasisha ushiriki wa Wadau mbalimbali kutoka Mikoa ya Dodoma,Singiida na mingine ya karibu katika Maonyeshi hayo wakiwemo wakulima na wafugaji.Amesema Waziri Bashe.
"Wengine ni wavuvi ,wasindikaji
wa mazao ya kilimo na mifugo na uvuvi,wauza Pembejeo za kilimo,Mifugo na uvuvi pamoja na Wadau mbalimbali wa Sekta ya Kilimo,"Amesema Bashe