Na Avelina Musa - Dodoma
Katika kukabiliana na Mabadiliko ya tabia ya Nchi, Mamlaka ya Hali ya hewa Tanzania (TMA)imeitaka jamii kufuatilia na kuzingatia taarifa inayotolewa na mamlaka ili kujiepusha na majanga yanayoepukika na kuzingatia Sheria ya Hali ya hewa Nchini.
Amesema tutumie taarifa inayotolewa na mamlaka ya Hali ya hewa kwa ajili ya maendeleo endelevu ya Taifa kwa ujumla.
Kauli hiyo imetolewa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania Dkt.Ladislaus Chang'a katika maadhimisho ya wiki ya Mazingira ya Mwaka 2024 Jijini Dodoma ambapo amewakaribisha wakazi wa Dodoma kufika katika Banda hilo ili kujiongezea maarifa kuhusiana na masuala mbali mbali ya Hali ya hewa.
Amesema kazi kubwa kama mamlaka ni kuendelea kuelimisha jamii kuhusu umuhimu wa huduma za Hali ya hewa na wajibu wa kila mwananchi kufuatilia taarifa Kwa ajili ya kujiimarisha na kuongeza ufanisi wa kuokoa maisha ya watu na Mali zao.
"Mazingira na Hali ya hewa ni vitu vinavyoenda sambamba ambapo Hali ya hewa inaathiri mazingira na mazingira inaathiri Hali ya hewa hivyo lengo ni kuielimisha jamii kuendelea kutunza mazingira,"Alisema dkt Chang'a.
Aidha,Dtk Chang'a amewataka watanzania kujua na kuzingatia Sheria za Mamlaka ya Hali ya hewa na 2 ya mwaka 2019 ambapo inatoa haki na wajibu wa kila mwananchi katika kuhakikisha Sheria ya Hali ya hewa inazingatiwa.
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania inashiriki kikamilifu katika Maadhimisho ya wiki ya Mazingira kwa mwaka 2024 yenye kauli Mbiu "urejeshwaji wa Ardhi, ustahimilivu wa hali ya Jangwa na ukame.
Mwisho.