Wakala wa usajili wa biashara na leseni(BRELA)umewataka Wananchi wote ambao wana biashara ama Kampuni kuhakikisha wanathibitisha usajili wao ili kuweza kupata haki za msingi Pamoja na Fursa za kibiashara kwa wawekezaji wa nje.
Afisa Usajili wa BRELA ,Gabriel Gilangay amesema hayo Juni 21 Jijini Dodoma katika Maonyesho ya Wiki ya maadhimisho ya Utumishi wa Umma yanayoendelea katika Viwanja vya Chinangali Park.
Gilangai amebainisha kuwa uthibitisho huo unatakiwa kufanyika kwa kujaza fomu namba 128 ambayo itaonyesha taarifa za mfanyabiashara huyo kutambulika jambo ambalo Ni muhimu kwa Mwananchi ambaye anatoa huduma za bidhaa mbalimbali kutokana na nchi hivi sasa kufunguka kumekuwa na wawekezaji wengi wakiingiq nchini hivyo wao huwa wanatafuta wafanyabiashara waliojisali ili kufanya nao kazi.
“Kwahiyo ndugu Waandishi Marina kwa namna gani hii ni fursa kwa wananchi ambao wa atakuwa kuichangamkia ili kupata Fursa Pamoja na haki mbalimbali ikiwemo kutqmbuliwa na Serikali,”Amesisitiza Afisa huyo
Sanjari na hilo amesema kupitia Wiki hiyo wanatoa elimu kwa wananchi kuhusu huduma wanazozitoa
Kama BRELA huku akiwashauri Wananchi kujaza fomu namba 128 kwaajili ya kutoa taarifa kuhusu usajili wao kama unafanya kazi au la na was ipo Fanyq hivyo mwisho wa siku Break itawafutia usajili.
Awali Kaimu Meneja Rasilimali na Utawala wa BRELA,Migisha Kahangwa amesema bado kuna changamoto kwa baadhi ya Wananchi kutoa huduma zao ambazo ni bidhaa bila kuzisajili Jambo ambalo sio jema.
Kahangwa amebainisha kuwa kila Mwananchi ana haki ya kutoa huduma kwa maana ya kufanya biashara lakini ili kuwa na uhakika ni muhimu kujisajili.
“Napenda kutoa wito kwa Wananchi wote ambao wamekuwa Wakijihusisha na kutoa huduma kwa wananchi kuhakikisha wanajisajili BRELA”,Amesema. Kuhangwa
Katika hatua nyingine amebainisha kuwa ili kukabiliana na changamoto hiyo wao BRELA,wamekuwa wakitioa elimu kwa Wananchi kutumia huduma za BRELA na hivyo Ni muhimu wachangamkie Fursa ya elimu kupitia maonyesho hayo ya wiki ya Utumishi wa Umma kupata Elimu kuhusiana na huduma wanazozitoa.
MWISHO