Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Disemba 01, 2023 amewasili mkoani Morogoro ambapo atahutubia katika maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya UKIMWI Duniani ambapo Kitaifa yanafanyika mkoani humo.
Kaulimbiu ya Maadhimisho ya mwaka wa 2023 ni *Jamii Iongoze Kutokomeza UKIMWI* ikiwa inasisitiza jamii kushiriki katika mapambano ya kutokomeza UKIMWI.