RAIS SAMIA ATUNUKIWA UDAKTARI WA HESHIMA
RAIS Samia Suluhu Hassan leo Desemba 28, 2023, ametunukiwa Shahada ya Heshima ya Uzamivu ya Usimamizi wa Utalii na Masoko katika Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) Tunguu Zanzibar.
Chuo hicho kimemtunuku Shahada hiyo kwa kutambua mchango wake wa kuifungua nchi kiuchumi kupitia sekta ya utalii.
