TANNA WATOA MKONO WA POLE HANANG,MUUGUZI ALIYEPOTEZA NDUGU ZAKE WATANO...

0

TANNA WATOA MKONO WA POLE HANANG, MUUGUZI PENDO ASIMULIA ALIVYOPOTEZA NDUGU ZAKE WATANO.

 

Chama cha Wauguzi Tanzania (TANNA) kimetoa mkono wa pole wa vifaa vya ujenzi  kwa waathirika wa mvua ya mafuriko iliyoambatana na maporomoko ya tope Wilayani Hanang Mkoani Manyara.

Makamu wa Rais wa Chama  TANNA  JANE BARARUKULULIZA amesema vifaa vya ujenzi vilivyokabidhiwa ni pamoja na mifuko  120 ya saruji, bati vyenye thamani ya Tsh. Milioni sita,laki mbi na elfu themanini(Tsh. 6,280,000) huku wakitembelea na kutoa mkono wa pole pia kwa Muuguzi Pendo Sephania aliyepoteza ndugu zake watano .

“Mkono wetu wa pole upo katika maeneo makuu mawili, tuna mkono wa pole ambao ni fedha tasilimu tunazowapa wauguzi wetu, tuna milioni moja na nusu tunampa Pendo Rajab ambaye amepoteza wanafamilia watano na tuna Tsh.laki tano ambayo tunampa Pendaeli  ambaye amepoteza nyumba na mali zilizokuwa ndani, lakini kama Wauguzi watanzania ni sehemu ya Watanzania kwa hiyo kama uongozi tunaungana kwa pamoja na kumshika mkono Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan tumetoa mchango utakaogusa waathirika wote  ikiwemo wauguzi wetu, tumetoa mifuko ya saruji 120 pamoja na bati”amesema.

Katibu tawala Wilaya ya Hanang Mwalimu Athumani Likeyekeye amekishukuru TANNA kwa kutoa msaada huo kwa waathirika.

 “Tunatamani watu wa Hanang warejee kwenye makazi yao kama watanzania wengine hiki mlichokifanya  ni kikubwa katika kuunga mkono jitihada za Mama Mungu awabariki sana sisi tunawashukuru sana pia kwa kujali familia za ndugu wauguzi wenzenu”amesema.

 

Muuguzi Pendo Sephania amesema alipoteza ndugu zake watano akiwemo mama yake mzazi,dada mkubwa pamoja na mtoto wake na kaka zake wawili hivyo ametumia fursa hiyo kushukuru chama cha Wauguzi Tanzania kwa kuwatia Moyo pamoja na kuishukuru serikali kwa kutoa Tsh. Milioni 5 kugharamia mazishi.

Ikumbukwe kuwa  Makamu wa Rais wa Chama   cha Wauguzi Tanzania (TANNA ) JANE BARARUKULULIZA Katibu Mwenezi Msaidizi PROSPER PROTAS  waliambatana na Muuguzi mkuu mkoa Manyara na viongozi   wa chama mkoa na wilaya kukabidhi vifaa  hivyo vya ujenzi..

TAZAMA VIDEO ZAIDI HAPA CHINI

Tags

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)