MAMA MJAMZITO AONGOZANE NA MWENZA WAKE WAKATI WA KUJIFUNGUA - MKUNGA

MUUNGANO   MEDIA
0

 

Mama mjamzito anapokwenda kujifungua anapaswa kuongozana na msaidizii aidha mwenza wake, mama, rafiki au mtu wa karibu na kuingia nae katika chumba cha kujifungua. 


Hayo yamesemwa na Bw. Shukran William, Afisa Mkunga kutoka Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Temeke wakati akiwasilisha muongoz mpya wa kuhudumia kina mama wakati wa kujifungua(Chati uchungu) kwa madaktari, wauguzi na madktari tarajali hospitalini hapo.


Muongozo huo, unaojulikana kama "Labour Care Guide," umefanyiwa marekebisho ili kuboresha huduma kwa wanawake wakati wa kujifungua. Mojawapo ya mabadiliko muhimu ni kuongezwa kwa kipengele cha msaidizi wakati wa kujifungua, ambapo mama mjamzito anapewa fursa ya kuwa na msaidizi wake anayempenda naye atakayeandamana nae hadi chumba cha kujifungulia.


Bw. Shukrani William aliendelea kufafanua, "Uwepo wa msaidizi wakati wa kujifungua unalenga kutoa msaada wa kihisia na kimwili kwa mama mjamzito. Tunataka kuhakikisha kuwa wanawake wanajisikia salama, na kuwa na msindikizaji wao wanapopitia uchungu wa uzazi."


uwasilishwaji wa muongozo huo uliambatana na kazi kwa vitendo ya namna sahihi ya kuhudumia mama mjamzito anapofika hospitalini. Washiriki walipata fursa ya kushuhudia igizo linaloonyesha madaktari na wauguzi jinsi ya kutoa huduma kwa usahihi, kuanzia kauli nzuri, vitendo sahihi, na huduma kwa ujumla.


Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Temeke inaendelea kujitahidi kutoa huduma bora na kuboresha uzoefu wa kujifungua kwa wanawake katika jamii na inatarajia kuanza kutumia muongozo huo ikiwa ni moja ya jitihada za kuhakikisha afya bora ya uzazi kwa mama na mtoto.

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)