CHUKUENI TAHADHARI DHIDI YA MAGONJWA YA MLIPUKO-DKT. SAMIA
Author -
MUUNGANO MEDIA
Ijumaa, Desemba 08, 2023
0
.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Wananchi wa Mji mdogo wa Katesh Wilayani Hanang Mkoani Manyara baada ya
kutokea maafa ya mafuriko.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan akimjulia hali mgonjwa katika Hospitali ya
Wilaya Hanang(Tumaini) mkoani Manyara .
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa amembeba mmoja watoto walio katika
kambi ya Waathirika wa Mafuriko Mji mdogo wa Katesh Wilayani Hanang Mkoani
Manyara.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwasalimia baadhi ya wagonjwa na Waathirika wa Mafuriko katika
moja ya Kambi Mji mdogo wa Katesh Wilayani Hanang Mkoani Manyara.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania akielekea kuwajulia hali Wagonjwa wakiwemo majeruhi wa mvua ya
mafuriko Katesh Wilayani Hanang Mkoani Manyara.
Mtaa
wa Katesh Sokoni Wilaya ya Hanang Mkoani Manyaraambapo soko lote lilifunikwa na tope
lililochangamana na takataka mbalimbaliambazo ni hatari kwa afya hivyokuwa nauwezekano wa kupata
Magonjwa ya mlipuko ikiwemo Kipindupindu.
Tahadhari
za Kiafya zimekuwa zikitolewa ikiwemo wananchi kutoingia kwenye maji hayo bila
kuvaa Kinga kwani ni hatari kiafya.
Wataalam kutoka Wizara ya Afya ,
MratibuWahudumu wa Afya Ngazi ya
Jamii(CHWs )wa kijiji chaJorodom Kati
wakitoa elimu ya kutumia vidonge vya kutibu maji na kutoa elimu ya Usafi wa
mazingira na matumizi ya vyoo. Elimu hii inatolewa nyumba kwa nyumba
Upatikanaji
wa Maji safi na salama baada ya kuchimbwa visima virefu Katesh Wilayani Hanang
Mkoani Manyara itasaidia kuepukana na Magonjwa ya kuhara na kutapika.
Uchimbaji
wa Visima hivi umefuatia baada ya mifumo ya miundombinu ya maji kuharibiwa na
mafuriko hivyo kusababisha kuchangamana na maji taka kutoka vyooni na Sehemu
zingine zisizo salama kwa afya.
Na.Elimu ya Afya kwa Umma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa wito kwa wananchi Mji mdogo wa
Katesh Wilaya ya Hanang Mkoani Manyara na Watanzania kwa ujumla kuendelea
kuchukua tahadhari za magonjwa ya mlipuko kwa kuzingatia kanuni za afya ikiwemo
matumizi ya maji safi na salama.
Dkt. Samia ametoa wito huo Disemba 7
,2023 wakati akizungumza na wananchi mji mdogo wa Katesh Wilayani Hanang
Mkoa Manyara baada ya Disemba 3, 2023 kukumbwa na maafa ya mafuriko
yaliyosababisha maporomoko ya udongo kutoka mlima Katesh na kusababisha madhara
makubwa ikiwemo majeruhi,vifo na upotevu wa mali.
"Jambo kama hili linapotokea
huwa yanatokea magonjwa ya mlipuko ,niwaombe wananchi wachukue hatua stahiki za
kuzingatia kanuni za afya pindi wanapotumia maji wazingatie kuepuka magonjwa ya
mlipuko ikiwemo kuhara "amesema.
Aidha, Rais Samia ametoa maagizo kwa
Wizara ya Afya kuhakikisha elimu na ufuatiliaji kwa kina inatolewa kwa
wananchi.
"Wizara ya Afya hakikisheni
elimu juu ya kujikinga na madhara yanayoweza kutokea kutokana na mafuriko
inatolewa pia kufuatilia kwa kina majeruhi mpaka kuhakikisha wanakuwa katika
hali ya kawaida"amesema.
Halikadhalika, Dkt.Samia ameagiza
kuhakikisha msaada wa Kisaiklojia unaendelea kutolewa pamoja na huduma za maji
safi na salama kuendelea kuimarishwa.
Hata hivyo,ametumia fursa hiyo
kuwashukuru wadau kwa kutoa msaada ambapo jumla ya Tsh.Bilioni 2.5 zimetolewa
na wadau kutoka nje ya nchi huku akielekeza zitumike kujenga makazi ya kudumu
kwa waathiriwa.