Timu ya Wawakilishi kutoka Wizara ya Afya, UNICEF, Jiji la Dar Es Salaam, Manispaa ya Ilala wakiwa katika Mtaa wa Buguruni Jijini Dar Es Salaam wakifuatilia jinsi zoezi la uraghibishi (uhamasishaji) wa Chanjo lilivyofanyika ambapo walipita nyumba hadi nyumba kuhakiki.
Na.Elimu ya Afya Afya Afya Umma.
Wito umetolewa kwa wazazi kuwa na desturi ya kufuatilia kadi za kliniki za watoto ili kuweza kufuata mtiririko sahihi wa chanjo za watoto ambazo husaidia kujikinga na magonjwa yanayoweza kuzuilika kwa Chanjo.
Hayo yamejiri katika Manispaa ya Ilala Mkoani Dar Es Salaam baada ya Uwakilishi kutoka Wizara ya Afya ,timu ya Watalaam wa Afya Manispaa ya Ilala pamoja na Uwakilishi kutoka Shirika la kuhudumia watoto Duniani(UNICEF) kutembelea kujionea zoezi la uraghibishi wa Chanjo katika Manispaa ya Ilala ikiwa ni katika utekelezaji wa Usimamizi Shirikishi wa Afua za Chanjo kupitia Mpango wa Human Centred Design (HCD)
Akizungumza katika zoezi hilo, Simon Nzilibili kutoka Sehemu ya Elimu ya Afya kwa Umma, Wizara ya Afya amesema zoezi la utoaji wa Chanjo nyumba kwa nyumba kwa watoto walio na umri wa miaka 5 limekuwa na mafanikio Wahudmu wa Afya ngazi ya Jamii wamekuwa Wakitembelea kaya zaidi ya 40 kwa siku.
“Kweli inatia moyo wakati mwingine wanatembelea kaya zaidi ya 40 na malengo tuliweka ni kaya 40 kwa siku na tuliona ni nyingi sana na kaya hizo unakuta zingine zina familia 5 mpaka sita ukija kujumlisha wanafikia zaidi ya familia 100 mpaka 170 kwa siku na leo wametebelea familia 172 tuendelee kuhamasisha jamii ili pasiwe na mtoto hata mmoja ambaye hajafikiwa huduma za chanjo”amesema.
Kwa upande wao baadhi ya Wahudumu wa Afya katika zoezi hilo la uraghibishaji wa Chanjo akiwemo Julita Magoti na Mambo Mdadike wamesema zoezi ni zuri huku wakitoa wito kwa wazazi kujenga desturi ya kufuatilia kadi za watoto kwani wanapofikisha umri wa miezi 6 ni muhimu kupata chanjo katika kuzuia magonjwa yanayozuilika kwa chanjo ikiwemo Surua.
Ikumbukwe kuwa hivi karibuni Mkuu Wilaya ya Ilala Mhe. Edward Mpogolo alizindua mfumo wa uraghibishaji wa Huduma za Chanjo katika Wilaya hiyo ambapo lengo zaidi ya watoto 2000 kupatiwa chanjo ambao hawakupata chanjo .