Na. Carlos Claudio, Dodoma.
Naibu
Waziri wa Kilimo Mhe. David Silinde ametoa rai kwa wadau wa kilimo nchini kuweka
mipango na vipaumbele ili kuhakikisha mkakati wa kilimo Ikolojia hai unatekelezwa
kwa ufanisi na kuleta tija katika jamii.
Mhe.
Silinde ametoa rai hiyo Jijini Dodoma wakati akifungua mkutano wa tatu wa kitaifa
wa kilimo Ikolojia Hai ambao unatarajia kufanyika kwa siku mbili huku wadau
mbalimbali wa kilimo wakishiriki katika mkuatano huo.
Amesema
pamoja na kujadili malengo mbalimbali mkutano huo utashuhudia uzinduzi wa
mkakati wa kilimo Ikolojia Hai kupitia wadau wote ndani na nje ya Tanzania
waliochangia rasilimali mbalimbali zilizopelekea ukamilishaji wa zoezi la
uandaaji wa mikakati wa huo.
“Mkutano
huu ukiwa umehudhuriwa na wadau wengi taasisi za serikali, taasisi zisizo za
kiserekali, wabia wa maendeleo wa ndani na nje ya Tanzania, sekta binafsi na
wawakilishi wa bara unaenda kutafakari kwa kina ili kutekeleza kwa vitendo
jitihada za kuendeleza kilimo Ikolojia hai katika taifa letu”amesema Silinde..
Kwa
upande wa kiongozi wa mradi kitovu cha Agroecology nchini Prof. Dismas Mwaseba
amesema kilimo cha kisasa hakijafanikiwa kwani bado kuna tatizo la njaa nchini
kutokana na mfumo wa kilimo hivyo kilimo Ikolojia kina fursa kubwa kwasababu ya
faida inayotokana na kilimo chenyewe ambacho kinazingatia maswala ya kijamii,
kiuchumi na mazingira pia.
“Kuna
umuhimu wa kuendeleza majidiliano na serikali ili kuwa na sera rafiki ambazo
zitasaidia muendelezo wa kilimo Ikolojia nchini Tanzania kwa maana kwamba ili
uweze kueneza kilimo hiki kuna jambo kubwa linahitajika, tunahitaji msukumo wa
kitaasisi ninaposema msukumo wa kitaasisi hapa nina maana maswala yote
yanayohusiana na sera, mipango, sheria mbalimbali zinahitajika ili tuweze
kufanikiwa katika swala hili,”amesema Prof. Mwaseba.
Naye
Mkurugenzi mtendaji wa Biovision African Trust Dkt. David Amudavi amesema
kilimo hai Ikolojia ni maisha pia ni chakula na wanahitaji kuona Afrika ikiwa
mahali salama na watu wanaishi maisha na mazingira ya afya nzuri kupitia kilimo
cha Ikolojia.
“Kilimo
hai kimewekwa nguli na viongozi wetu wa nchi zote za Afrika. Mwaka wa 2010
mawaziri wote wa kilimo walithibitisha sheria ya kusema kwamba kilimo hai
kipatiwe nafasi katika nchi zetu zote za Afrika na mwezi January 2030 viongozi
wataweka sahihi,” amesema Dkt. Anudavi