Na Carlos Claudio, Dodoma.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu Mhe.
Jenista Mhagama ametoa msisitizo kwa wakina baba kujitokeza kwa wingi katika
zoezi la upimaji wa hiari wa Virusi Vya Ukimwi kuelekea maadhimisho ya siku ya
Ukimwi duniani.
Mhe. Mhagama ameyasema hayo leo Novemba 14,2023 Jijini Dodoma wakati
akizungumza na waandishi wa habari kuelekea maadhimisho ya siku ya UKIMWI
duniani yatakayo fanyika kitaifa mkoani Morogoro Desemba 1 huku yakitanguliwa
na wiki ya UKIMWI itakayozinduliwa Novemba 24 mwaka huu.
“Tunatumia maadhimisho haya katika kuhakikisha kwamba tunatoa taarifa za
nchi zinazohusu udhibiti wa VVU na Ukimwi lakini pia katika maadhimisho haya na
wiki nzima tunaitumia pia kutoa huduma za upimaji na hasa upimaji wa hiari wa
VVU na hapa leo nimeanza kwa kuhamasisha tuanze kukumbuka kwamba ni wiki ambayo
angalau kila mmoja kwa hiari yake anaweza kuitumia kama wiki ya kupima afya
yake”.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi mtendaji wa Tume ya Taifa ya kudhibiti UKIMWI
Tanzania (TACAIDS) Dkt. Jerome Kamwera amesema kuwa wanaume wengi nchini
hupoteza maisha kutokana na ugonjwa huo kwakuwa hawana utamaduni wa kutambua
hali zao.
“Kwenye tafiti zote wanaume wapo nyuma lakini pia hata ukiwa unaangalia
takwimu ambazo zinaonysha matokeo ya tiba wanaume kwa ujumla ni wavivu sana
kwenda kupata huduma za tiba na kwa msingi huo basi ukuangalia hata matokeo ya
tiba kwa wanaume ni mabaya kuliko kwa wanawake wote tunajua kwamba kiwango cha
maambukizi kipo juu kwa wanawake kuliko wanaume lakini naomba nikwambie kwamba
wanaume ndo wanakufa zaidi kwa magonjwa yanayotokana na Ukimwi kuliko
wanawake.”
“Kama hauendi kwenye huduma na kama hauendi kwenye huduma eitha
utapelekwa ukiwa na hali mbaya na matokeo yatakuwa ni mabaya kwaio tafiti zote
zinaonyesha hivyo kwa kipindi chote na ndio maana tunaweka msisitizo kwamba
sasaivi wanaume tujitokeze tupime ili tujue hali zetu twende tukapate huduma
ambazo zinafanana na hali zetu.” amesema Dkt. Kamwera.