Wananchi hao wametoa pongezi hizo wakati wa zoezi la kambi maalumu ya matibabu ya Macho ikiwemo upasuaji wa mtoto wa jicho inayoendesha na kufadhiliwa na Shirika la Hellen Keller kupitia kampeni ya Cataract kwa kushirikiana na Hospital ya Rufaa ya Kanda ya Mbeya pamoja na Hospital ya Wilaya ya Wanging'ombe ambapo kupitia kampeni hiyo jumla ya wananchi 900 wenye matatizo mbalimbali ya macho wanatarajiwa kupatiwa huduma mbalimbali ikiwemo dawa na upasuaji huduma hiyo inatolewa na madaktari Bingwa wa Macho kutoka katika Hospital ya Kanda ya Mbeya.
WANANCHI WANGING'OMBE WANOGESHWA MATIBABU BURE YA MACHO
Jumanne, Novemba 28, 2023
0
Wananchi Wilayani Wanging'ombe Mkoani Njombe wamefurahishwa na kupongeza hatua ya Serikali kwa kushirikiana na Shirika la Hellen Keller Intl kwa kuweza kuwapatia matibabu ya macho bila malipo.
Tags