Na. Gideon Gregory, Dodoma.
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU Mkoa wa Dodoma imetoa taarifa kuhusu utendaji kazi wake kwa kipindi cha miezi mitatu kuanzia mwezi Julai hadi Septemba 2023 ambapo wamefanya kazi ya uzuiaji wa Rushwa kupitia uchambuzi wa mifumo ya ufuatiliaji wa miradi ya maendeleo.
Akiwasilisha taarifa hiyo mbele ya waandishi wa habari leo Novemba 30,2023 Jijini Dodoma Mkuu wa TAKUKURU John Joseph amesema kuwa wamefanya ufuatiliaji wa utekelezaji wa miradi ya maendeleo 64 yenye thamani ya zaidi ya bilioni 27.10 kutoka katika sekta tano za Elimu, Ujenzi, Afya, Maji, Utawala, Ustawi wa jamii na mifugo.
“Mchanganuo wake kwa kila sekta ni Elimu ni miradi 51, Ujenzi ni mradi 1, Utawala 1, Ustawi wa jamii 1, Mifugo 2, Maji 5 na Afya ni miradi 3”, amesema Joseph.
Amesema ufuatiliaji huo unefanyika sanjari na matumizi ya fedha za mpango wa maendeleo kwa Ustawi wa taifa na mapambano dhidi ya UVIKO-19 ambapo baadhi ya miradi yake imefuatiliwa.
“Katika ufuatiliaji huu wa miradi ya maendeleo tumebaini kuwepo kwa mapungufu kadhaa katika miradi 28 yenye thamani ya jumla ya shilingi bilioni tano milioni mia moja sitini na mbili laki mbili sabini na nne mia tano ishirini,”amesema.
Amebainisha kuwa mapungulfu hayo ni pamoja na uekezaji wa majengo kwa kutumia mabati yaliyochini ya kiwppango (ubora hafifu) , baadhi ya majengo kuwa na nyufa nyingi, wazabuni kuliplwa fedha nyingi nje ya mkataba, kulipwa kabla ya kufikisha vifaa, kulipwa fedha nankuwasilisha vifaa pungufu.
Aidha Joseph ameongeza kuwa TAKUKURU imepokea jumla ya malalamiko 165 kati ya hayo 53 hayakuhusu rushwa hivyo walalamikaji 30 walielimishwa, 10 yamehamishiwa Jeshi la Polisi na 13 walalamikaji wake walishauriwa namna bora ya kutatua malalamiko waliyokuwa nayo.
Sanjari na hayo ametaja vipaumbele vyao Kwa kipindi cha mwezi wa Oktabo mpka Disemba kuwa ni kufanya uchunguzi katika tuhuma zilizoainishwa katika taarifa ya mkaguzi na mdhibiti mkuu wa hesabu za serikali, malalamiko ya matumizi mabaya ya ofisi katika idaroa ya Ardhi katika Jiji la Dodoma na tuhuma nyingne kadri zitakavyo bainika.
Pia ametoa wito kwa wananchi kushiriki katika mapambano dhidi ya Rushwa kwani ni wajibu wa kikatiba ibara ya 9(H) na wakumbuke kuwa Rushwa ni ni adui wa taifa kama ilivyo ujinga, maradhi na umaskini.