NDEJEMBI: KATESH ITAJENGWA BARABARA YA LAMI KM 10.

MUUNGANO   MEDIA
0

 


OR-TAMISEMI.

NAIBU Waziri Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mhe. Deogratius Ndejembi amesema serikali kupitia kwa Wakala wa Barabara za Mijini na Vijijini (TARURA) imeanza utekelezaji wa ahadi ya Mhe. Rais kwa wananchi wa Katesh mkoani Manyara ya kujengewa barabara za lami za ndani zenye urefu wa kilometa 10.


Mhe. Ndejembi ametoa kauli hiyo Novemba 9, 2023 bungeni jijini Dodoma alipokuwa akijibu maswali ya wabunge ambapo amesema Sh. Milioni 941.9 zimetengwa katika mwaka wa fedha 2023/24 kwa ajili ya ujenzi wa kilometa 1.2 na utekelezaji wake umefikia asilimia 30.


"Serikali kupitia kwa TARURA imeanza utekelezaji wa ahadi hiyo ambapo kwa mwaka wa fedha 2021/22 jumla ya Sh. milioni 470 zimetumika katika ujenzi wa barabara kilometa 1.12 kwa kiwango cha lami.Katika mwaka wa fedha 2022/23 jumla ya kilometa 0.7 zimetengwa kwa kiwango cha lami ambapo kiasi sh Sh. Milioni 499 kimetumika kwa ajili ya ujenzi huo," amesema.


Aidha, amesema serikali itaendelea kutenga bajeti kulingana na upatikanaji wa fedha ili kukamilisha ujenzi wa kilometa 10 za barabara hiyo kwa kiwango cha lami.

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)