MAAFISA TARAFA NA WATENDAJI KATA ZUIENI MIGORORO YA ARDHI.

MUUNGANO   MEDIA
0

 

OR-TAMISEMI.

Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Mhe. Dkt. Batilda Buriani amewataka Maafisa Tarafa na Watendaji wa Kata kuhakikisha wanakuwa mstari wa mbele katika kuzuia migogoro kati ya Serikali na wananchi hasa migororo ya ardhi kwa kuwa mingi inaanzia kwenye ngazi zao.


Mhe. Buriani ameyasema hayo leo alipokuwa akifunga Mafunzo ya viongozi hao yaliyofanyika kwa siku mbili   mkoani humo.


Amesema  migogoro ya ardhi imekuwa ni changamoto kubwa katika maeneo mengi na kuwaelekeza  maafisa hao kua  wazalendo na imani na  kutumia misingi ya haki na sio upendeleo pale linapokuja suala la uuzaji wa ardhi za watu.

"Baadhi ya vijiji wameuza ardhi na wananchi wanalalamika hii inasababisha  baadae migogoro kati ya Serikali na wananchi wake mnapaswa kuwa  na maadili mnapotekeleza majukumu yenu,"amesema.


Aidha, amesisitiza viongozi hao kuwa na  ushirikiano mzuri  na wananchi wanaowaongoza kwenye maeneo yao.





Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)