MAGARI MMEPATA MSIWE NA KISINGIZIO - MCHENGERWA.

MUUNGANO   MEDIA
0

 



Na. Gideon Gregory, Dodoma.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Mohamed Mchengerwa amewataka Maafisa Elimu Sekondari wa Halmashauri kutekeleza majukumu yao ya Usimamizi na Ukaguzi kwani sasa hawatakuwa na kisingizio cha kukosa usafiri kwa kuwa magari waliokabidhiwa yatarahisisha katika utekelezaji wa majukumu yao katika maeneo mbalimbali ya shule ndani ya Halmashauri zao.

 

Waziri Mchengerwa ameyasema hayo Jijini Dodoma wakati wa hafla ya kukabidhi magari  36 iliyofanyika katika viwanja vya shule ya Sekondari Dodoma huku akiwataka Kuongeza  jitihada katika kutekelezwa majukumu yao.


Halikadhalika, Mhe.Mchengerwa amewata Maafisa Elimu hao kusimamia vyema suala la nidhamu, kuongeza zaidi ufaulu pamoja na kutanguliza maslahi ya taifa mbele.


“Misingi hii ya maslahi ya taifa izungumzwe sana katika kila halmashauri, katika kila maeneo ambayo tumejenga shule zetu, katika kila maeneo ambayo serikali ya awamu ya sita inaendelea kuongeza na kuboresha miundombinu ya elimu katika maeneo yenu”,amesema Waziri Mchengerwa.


Akizungumza kabla ya kukabidhi magari kwa Maafisa Elimu Sekondari Rais  wa 31 wa Umoja  wa  Mabunge ( IPU )na Spika wa Bunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson amewapongeza wabunge kwa hoja zao wanazopeleka Bungeni kwani ndio zimepelekea Serikali iweze kuchukua hatua hiyo ya kuwapatia magari.













Tags

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)