KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA NISHATI NA MADINI YAIPONGEZA WIZARA YA NISHATI KWA KAZI NZURI YA KUKAMILISHA UJENZI WA MIUNDOMBINU YA UMEME SGR.

MUUNGANO   MEDIA
0

 


Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini imeipongeza Wizara  na Taasisi yake ya  TANESCO kwa kazi nzuri waliyoifanya ya kukamilisha ujenzi wa Mradi wa njia ya Kusafirisha Umeme wa Msongo wa KV 220 kutoka Kinyerezi (Dar-es-Salaam hadi Kingolwira (Morogoro) yenye urefu wa Kilomita 160 ambayo itakuwa na umeme wa uhakika utakaolisha vituo vyote vinne vya kupoza umeme vilivyopo katika reli ya kisasa.


Pongezi hizo zimetolewa tarehe 11 Novemba, 2023 na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini Mhe. Dkt. David Mathayo wakati Kamati hiyo ilipotembelea Kituo cha Mradi wa Njia ya Kusafirisha Umeme wa Msongo wa KV 220 kutoka Kinyerezi (Dar-es-Salaam hadi Kingolwira (Morogoro) kwa ajili ya uendeshaji wa Treni ya Mwendokasi na kukamilisha  kazi hiyo kwa asilimia mia moja.


Kamati hiyo pia , imetembelea Kituo cha Kupokea na Kupoza Umeme cha Msamvu na kuelezea kufurahishwa kwake na utayari wa Kituo hicho kuhudumia miundombinu kwa ajili ya treni ya Mwendokasi (SGR).


Akizungumza wakati wa mkutano na Waandishi wa Habari, Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini Mhe. Dkt. David Mathayo  ameiomba Serikali kutoa elimu kwa Wananchi walio jirani na maeneo ya Mradi ili kuepuka madhara yanayoweza kujitokeza.


"Ninamshukuru sana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia  Suluhu Hasan ,kwa kutenga fedha kwa ajili ya kukamilisha Mradi wa Miundombinu ya Mradi wa SGR.. Pia tumejionea wenyewe Mradi wa Umeme kutoka Kinyerezi mpaka Msamvu umekamilika kwa asilimia mia moja.Kamati tumeridhishwa sana na Mradi ambao Serikali imefanya." Amesema Mwenyekiti huyo.


Dkt. Mathayo amesisitiza kuwa maeneo ambayo Treni ya Umeme imepita ni vyema Serikali kuongeza ulinzi kwa kushirikiana na Serikali za  Mitaa kuhakikisha  Wananchi hawapiti katika maeneo yaliyowekewa uzio ili kuzuia ajali ambazo zinaweza kutokea


Dkt. Mathayo amelihimiza  Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO)  kukamilisha kazi katika maeneo machache  yaliyobakia ambayo ni asilimia moja kwa kushirikiana na Shirika la Reli Tanzania (TRC) ili kukamilisha mambo yaliyobakia.


Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Nishati Mhe. Judith Kapinga amesema Wizara ya Nishati itaongeza usimamizi kuhakiksha Mradi unakamilka kwa Wakati kwa maeneo yaliyosalia.

Tags

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)