"Kamati inaipongeza Serikali kwa kuchukua hatua kuandaa na kuleta muswada wa bima ya afya kwa wote wa mwaka 2022 ambao unalenga kuweka utaratibu utakaowawezesha wananchi kupata huduma bora za afya bila kikwazo cha fedha" amesema Mheshimiwa Stanslaus Nyongo Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Afya na Masuala ya Ukimwi
Mhe. Nyongo amesema Sheria inayopendekezwa ni muhimu sana kwa maendeleo ya mwananchi mmoja mmoja na taifa kwa ujumla, kutungwa kwa Sheria hii kutawawezesha wananchi kunufaika na huduma za afya katika vituo vyote, kuongeza kiwango cha kuishi.
"Serikali ina dhamira ya kutambua ma kugharamia huduma za bima za afya kwa watu wasio na uwezo ambapo kamati ilishauri Serikali kuanzisha mfuko maalum (Equit fund) ambao utakua vyanzo mahususi vya fedha na vyenye uhakika" amesem Mhe. Nyongo.
Ameitaka Serikali kuweka juhudi katika kutoa elimu mara kwa mara kwa wananchi kuhusu umuhimu wa kijiunga na skimu za bima ya afya, utaratibu wa ugharamiaji wa huduma za afya kwa kutumia bima za afya.