Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe Ofisi ya Rais - TAMISEMI Dkt. Wilson Mahera amewaelekeza Waganga Wakuu wa Mikoa, Wakurugenzi na Waganga Wakuu wa Wilaya kuhakikisha matumizi ya Mfumo wa Uendeshaji na Usimamizi wa Huduma za afya (GoTHOMIS) kwenye vituo vya kutolea huduma za Afya unakua endelevu.
Dkt.Mahera ameyasema hayo wakati akifunga mafunzo ya Maafisa TEHAMA wa Mkoa wa Dodoma kuhusu Mfumo wa GOTHOMIS tarehe 24.11.2023 Jijini Dodoma kwenye ukumbi wa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma.
“Tumepata vifaa na rasilimali kupitia mradi ambavyo vitasaidia kupanua matumizi ya mfumo wa GOTHOMIS mkoani Dodoma, na sasa ni jukumu letu kuhakikisha kwamba tunatumia vyema rasilimali hizi na maarifa tuliyoyapata kuhakikisha huduma za Afya zinatolewa kupitia mfumo”amesema Mahera.
Sasa mfumo huo sasa ukawe endelevu na utumike ipasavyo na nimeskia kuna baadhi ya vituo vinawekewa mfumo na kisha kutoutumia ipasavyo ama kuacha kuutumia baada ya muda fulani kwa maslaho binafsi hawa hatutowavumia.
Dkt. Mahera amesema mafunzo haya yamewajengea uwezo ili mkatumie mfumo na kuhakikisha vituo vyote vya kutolea huduma za afya vinawekewa mfumo huu ikiwa ni pamoja na vile vituo vambavyo haviko kwenye mradi.
“Zoezi la kufunga mfumo na kutoa mafunzo lianze mara moja pindi tu vifaa vitakapofika kwenye vituo vyetu vya kutolea huduma ambapo vifaa hivyo vinatarajiwa kufika mwishoni mwa Disemba, 2023 au mwanzoni mwa January, 2024 “amesema Mahera.
Pia amewaagiza kuvainisha vituo ambavyo haviguswi kabisa na mradi kwa namna yoyote kuhakikisha pia vinatengewa fedha kwa ajili ya kuviwekea mfumo wa GOTHOMIS.Aidha inapotokea changamoto yoyote ya mfumo vituoni muhakikishe inatatuliwa kwa wakati na kuhakikisha Viongozi mnatumia data za mfumo katika kufanya maamuzi mbalimbali.