Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia Elimu Ofisi ya Rais - TAMISEMI Dkt. Charles Msonde ametembelea shule zinazojengwa kupitia mradi wa BOOST na SEQUIP wilayani Rufiji kukagua maendeleo ya ujenzi wa miundombinu hiyo jana tarehe 29.11.2023.
Katika ziara hiyo amezitaka Halmashauri zote zonazotekeleza miradi hiyo kuhakikisha wamekalisha ujenzi ifikapo Disemba 30,2023 ili miundombinu hiyo iweze kutumiwa na wanafunzi watakaonza masomo yao Januari,2024.