ACFET KUAFANYA MKUTANO WAKE JIJINI ARUSHA KUANZIA NOVEMBA 6-10 MWAKA HUU.

MUUNGANO   MEDIA
0

Na. Gideon Gregory, Dodoma.

Taasisi ya Wataalamu dhidi ya Rushwa na Ufisadi Tanzania (ACFET) inatarajia kufanya mkutano wake jijini Arusha kuanzia Novemba 6-10,2023 ambapo utahusisha watumishi kutoka taasisi mbalimbali kutoka nchini na nje ya nchi.


Hayo yamebainishwa leo Novemba 2,2023Jijini Dodoma na Rais wa taasisi hiyo Ali Mabrouk Juma wakati akizungumza na waandishi wa habari huku mgeni rasmi katika ufunguzi akitarajiwa kuwa Waziri anayeshughulikia masuala ya utawala bora kutoka Zanzibar Mhe. Haroun Ali Suleiman na siku ya kufunga atakuwa Mhe. Gerorge Simbachawene.


“Mada kuu katika mkutano huu itakuwa ni mapambano dhidi ya rushwa na ufisadi katika kujenga uchumi lakini pia katika kusimamia miradi ya maendeleo kwahiyo hii ndio mada kuu katika mkutano huu,” amesema.


Sanjari na hayo ameongeza kuwa kazi kubwa inayofanywa na taasisi hiyo ni kutoa elimu kwa wananchi pamoja na taasisi mbalimbali na kupeleka wataalamu wengine nje ya nchi kwenda kupata ujuzi zaidi katika kukabiliana na changamoto ya rushwa na ufisadi.


“Baada ya kuwapeleka wataalamu hawa kwenda kupata ujuzi Marekani, hivi sasa tumeandaa Mazingira ya wao kupata elimu hapa hapa nchini kutokana na gharama za kuwapeleka nje ya nchi kuwa kubwa,”amesema.

Kwa upande wake makamu wa Rais ACFET Stephen Agwanda amesema kuwa taasisi hiyo pia inaandaa wataalamu na wanapokuwa wameivaa wanazishawishi taasisi mbalimbali kuwa na wataalamu wanawezesha mapambano ya rushwa na ufisadi yanakomeshwa katika maeneo yao.


“Kwahiyo wanapokuwa wameajiriwa katika maeneo hayo kazi yao ni kuweka mifumo dhabiti ya kuhakikisha hatufikii mwisho mpaka mmepata tatizo ndiyo muanze kwenda kwenye vyombo vya uchunguzi lakini pia taasisi yetu ina mashirikiana makubwa na vyombo vya uchunguzi kama TAKUKURU,”amesema.

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)