RAIS WEAH KUCHUANA NA WAGOMBEA 19 UCHAGUZI LIBERIA.

MUUNGANO   MEDIA
0

 

Rais George Weah wa Liberia anatazamiwa kugombea muhula wa pili katika uchaguzi wa rais unaotazamiwa kufanyika kesho Jumanne.

Rais wa Liberia George Weah anatazamiwa kuchuana na wagombea 19 katika kinyang'anyiro cha kuwania kiti cha urais nchini humi, ambao pia itashuhudiwa wananchi wa Liberia wakiwachagua wabunge. Kwa mujibu wa Tume ya Uchaguzi, Waliberia milioni 2.4 wametimiza masharti kushiriki zoezi hilo la kidemokrasia.

Rais Weah anawania muhula wa pili wa miaka 6 kupitia muungano tawala wa Coalition of Democratic Change (CDC). Wagombe wawili wakuu wanaotazamiwa kumpa ushindani mkali ni Naibu Rais wa zamani, Joseph Nyuma Boakai na mfanyabiashara maarufu Alexander Cummings. 


Ingawaje Weah, 57, anasisitiza kuwa kazi kubwa aliyowafanyia Waliberia hasa katika kuboresha sekta ya elimu na kuimarish miundumsingi itamsaidia kushindi kiwepesi muhula wa pili, lakini wakosoaji wake wanahisi kuwa hajafanya mengi tangu aingie madarakani baada ya uchaguzi wa mwaka 2017.


Baada ya kushika rasmi hatamu za uongozi mnamo Januari mwaka 2018, rais huyo wa Liberia aliahidi kupambana na ufisadi ulioenea nchini humo na kuboresha uchumi wa nchi hiyo.

Hata hivyo wakosoaji wake wanasema uchumi wa Liberia ungali katika hali ya mdororo, thamani ya sarafu ya nchi hiyo inaendelea kushuka na kiwango cha ughali wa maisha kinazidi kupanda. Aidha ukosefu wa ajira umeongezeka kwa kiwango ambacho hakijawahi kushuhudiwa na akiba ya nchi ya fedha za kigeni ni haba mno hivi sasa kuliko wakati wowote ule.


Si vibaya kuashiria hapa kuwa, Liberia ilitumbukia kwenye lindi la vita vya wenyewe kwa wenyewe kuanzia mwaka 1989 hadi mwaka 2003 vilivyoua mamia ya maelfu ya watu.

Tags

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)