Amesema Serikali tayari imeshapeleka fedha kwenye kila Halmashauri kwa ajili ya kulipa stahiki za watumishi hao lakini mpaka leo kuna watumishi wa ajira mpya ambao hawajalipwa fedha za kujikimu, hii sio sawa watumishi wote walipwe fedha za zao kabla ya Oktoba 30, 2023.
"Fedha za kujikimu ni haki ya kila mwajiriwa mpya sasa, kwanini usilipe na fedha unayo kama kuna changamoto yeyote iwasilishwe ila sio kukaa na fedha na kuacha hawa watumishi wakihangaika, walipwe mara moja." amesisitiza Mhe. Mchengerwa.
Kwa mwaka wa fedha 2022/23, Serikali iliajiri watumishi wapya wa kada ya Ualimu na Afya ambapo kwa Kada ya Ualimu ni watumishi 13,130 na Afya ni watumishi 7,192 na wote wamekwisharipoti kwenye vituo vyao vya kazi.
Imetolewa na:
Nteghenjwa Hosseah
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Ofisi ya Rais –TAMISEMI
03.10.202