Na. Asila Twaha, Iringa.
Timu ya wanawake ya kuvuta kamba TAMISEMI mapema imecheza mechi dhidi ya timu ya mashtaka na kuifunga timu ya MASHITAKA kwa pointi 2-0 kwenye mechi iliyochezwa mapema leo asubuhi.
Mara baada ya ushindi Kocha wa timu ya TAMISEMI Chedieli Masinga amesema hadi sasa wanaendelea kufanya vizuri ambapo mpaka sasa mechi zote walizopangiwa wameshinda na tayari wanapointi 4 muhimu katika hatua ya makundi na zimebaki mechi mbili kuingia hatua ya robo fainali.
"Mchezo huu kila raoundi ni dakika moja sawa na sekunde 60 kwaiyo unahitaji umakini na mazoezi "amesema Chediel.