Tume ya nguvu za Atomiki (TAEC)Tanzania imesema imejiandaa katika kukabiliana na maafa kwani kuna uwezekano mkubwa wa kutokea mlipuko na janga la kinyuklia .
Hayo yameelezwa leo Oktoba 13 Jijini Dodoma na Mtafiti Mwandamizi toka Tume hiyo,Jerome Muimanzi wakati akizungumza na Waandishi wa habari katika maonyesho ya Kongamano la maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya kupunguza madhara ya maafa
Muimanzi amebainisha kuwa kutokana na hilo,wao kama Tume Sheria inawataka waandae Mpango Mkakati wa kudhibiti majanga pale yanapotokea ili kuwalinda wananchi.
Aidha.,Mtafiti huyo,amefafanua kuwa kutokana na Vyanzo vya mionzi kuna uwezokano mkubwa wa kutokea mlipuko wa mionzi au mlipuko wa kinyuklia hivyo wamekuwa wakishirikiana na shirika la nguvu za Atomu Duniani ili miongozo mbalimbali inapotoka inayohusiana na majanga waweze kushiriki na kuwa na utayari pale linapotokea janga nakuweza kulikabili.
“Sisi Tume ndio tuna jukumu la kusimamaia matumizi sahihi na salama ya mionzi nchini hivyo tuna jukumu la kuhakikisha tunawalinda wananchi wasipate madhara yatokanayo na mionzi sio tu kwenye matumizi hata pale linapotokea janaga kla kitaifa na kimataifa”,Amesisitiza.
“Hii inatuandaa kuwa na utayari yani pale linapotokea janga tuwe na uwezo wakukabiliana nalo, na tunashirikiana na Serikali kuandaa Sera na Mipango mikakati ya matumizi salama ya mionzn ili wasipate madhara yatokanayo na mionzi”,amesema Muimazi.