RAIS SAMIA AZINDUA SHULE ZA MRADI WA BOOST ZA TRIL.1.5.

MUUNGANO   MEDIA
0

 


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amezindua shule ya Msingi Imbele iliyojengwa katika Manispaa ya Singida mkoani Singida kwa niaba ya shule zote zinazojengwa kupitia mradi wa kuimarisha Elimu ya Awali na Msingi (BOOST).


Dkt. Samia amezindua shule hiyo leo tarehe 15.10.2023 wakati wa ziara yake mkoani Singida ikiwa ni mradi wa kwanza tangu alipopowasili mkoani humo.


Amesema amezindua mradi huu ni kwa niaba ya miradi mingine yote kama hii inayojengwa nchini na itasaidia watoto wetu waweze kupata elimu bora.

“Watoto wetu kazi yenu sasa ni kusoma kwa sababu shule nzuri mnazo na utaona kwenye Mradi huu wa BOOST tumejenga kuanzia madarasa ya awali hivyo mtoto akiwa na umri kuanzia miaka 4 apelekwe hapo ili aandaliwe kuanza darasa la kwanza; 


Pia ametoa rai kwa Wazazi na walezi wote kuhakikisha kuwa watoto wenye umri wa kwenda shule wanapelekwa shule na wanasoma mpaka kumaliza masomo yap pia ameitaka jamii kuitunza miradi hiyo ili iweze kunufaosha na vizazi vijavyo.


Akizungumza katika hafla hiyo Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Mohamed Mchengerwa amesema mradi huu umeanza kutekelezwa mwaka 2021 na kwa mwaka huu wa fedha shule mpya za msingi 302 zinajengwa, vyumba vya madarasa 2,929 yakiwemo ya mfano ya Elimu ya Awali 368, matundu ya vyoo 5,131, nyumba za Walimu 41, mabweni 2, na majengo ya Utawala 302.

Na mpaka september,2023 tumeshatoa Fedha shilingi  Bil. 230 na shule za msingi zilizokamilika mpaka sasa ni 194, madarasa ya awali 364, madarasa ya shule za msingi 2,303 na zingine ziko katila hatua mbalimbali za ujenzi wake’.


Mradi huo unaotekelezwa kwa kipindi cha miaka mitano utagharimu shilingi Trilioni 1.5 na unalenga kuimarisha Elimu ya awali na msingi nchi nzima.

Tags

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)