Na Gideon Gregory, Dodoma.
Mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 50 anayefahamika kwa jina la Hasna Bakari ametoroka nyumbani kwake baada ya kuzidiwa na mikopo maarufu kama vikoba, mwanamke huyo ambaye ni mkazi wa mtaa wa Mazengo kata ya Chang’ombe Jijini Dodoma alitoweka tangu Oktoba 4,2023 majira ya saa 12 jioni.
Akizungumza na Muungano Media leo Oktoba 9,2023 nyumbani kwake mume wa mwanamke huyo Nuru Hassan (64) amesema kuwa mama huyo amekuwa akichukua mikopo pale anapotoka kwenda kwenye shughuli zake ili hari mwanamke huyo hana kazi yoyote anayofanya ya kumuingizia kipato.
"Mimi ninaenda kwenye shughuli zangu nayeye anaenda kwenye mambo yake ya kuchukua mikopo, sasa hii mikopo anapokwenda kuichukua mimi sina taarifa anaenda anakopa huko anapojua na marafiki zake, sasa mara inapofikia ukingoni sasa imeshindikana kama hivi imeshindikana ameniachia madeni,"amesema Bw. Hassan.
Aidha ameongeza kuwa hiyo ni mara ya tatu mwanamke huyo anachukua mikopo na akishindwa kulipa anakimbia jambo lililomfanya Bw. Hassan kuitafuta Muungano Media ili aweze kupatikana na kurudisha fedha hizo.
"Hii ni mara ya tatu mara ya kwanza alikopa akakimbia na aliacha mtoto wetu wa kwanza ana umri wa miaka minne kwasababu sasa hivi tuna watoto saba nikaenda kutoa taarifa kwenye vyombo vya habari hadi magazeti yalitoa taarifa yake mpaka leo hii gazeti ninalo ndani, mara ya pili ilikuwa mwaka 2012 na hii ni mara ya tatu kwakweli hii changamoto inaniumiza sana hadi watoto wameisha mchoka mama yao na mikopo,"amesema.
Kwa upande wake mwenyekiti wa mtaa wa Mazengo Abdallah Ally amedhibitisha kupokea taarifa hizo na kuwaomba wanaotoa huduma kuwashirikisha watu wote katika utoaji wao wa huduma kwani wakinamama ndiyo wamekuwa akiathirika pakubwa na suala la mikopo.
Aidha ametoa ushauri kwa wanaokoposha kuwa wawazi katika kuelezea ukweli juu ya athari zinazoweza kujitokeza na kuweza kuwashirikisha wenza wao.
"Wenzetu basi wanapotoa huduma hizi tunaomba basi tuwe tunashirikishana na hasa hawa wakina mama ndiyo wamekuwa wakiadhirika zaidi na hii mikopo na kibaya zaidi wanawake hawa wanapeleka wanaume ambao sio sahihi basi tunaomba wawe wanapeleka vyeti vya ndoa ili kudhibitisha kweli huyo aliye mleta ni mume wake harari,"amesema Mwenyekiti.
Naye afisa Mtendaji wa mtaa huo Geofrey Nkinda amesema kuwa moja kati ya madhara ya natoweza kujitokeza katokeza kwa wale wanao chukua mikopo kihorera ni pamoja na kupoteza mali zao na kufirisiwa.