Na. Asila Twaha, Iringa.
Michezo ya SHIMIWI imeendelea kupamba moto katika viwanja mbalimbali Mkoani Iringa ambapo timu mbalimbali zimeendelea kuonyeshana ubabe ambapo timu ya wanawake netiboli TAMISEMI imeipiga kichapo timu MASHTAKA goli 25 -8.
TAMISEMI imeendelea kung'ara baada ya majira ya asubuhi kushinda mchezo wa kuvuta kamba dhidi ya MASHTAKA kwa pointi 2-0
Kichapo walichozea timu ya MASHTAKA kilionekana katika dakika 20 za kwanza ilipofunga goli 13- 2 na hadi mchezo unaisha TAMISEMI ilitoka mbabe kwa goli 25-8.
Kocha wa TAMISEMI Maimuna Kitete amesema bado wanaendelea na mashindano na bado wanaendelea na darasa la kufanya mazoezi sababu kilichowafanya kushiriki mashindano ya SHIMIWI sio tu kwa kufanya mazoezi ya afya kama watumishi bali pia ni kuhakikisha wanakuwa washindi.
" michezo hujenga afya,umoja,kujuana,kushirikia lakini pia ni ajira" amesema Maimuna
Ametoa wito kwa wachezaji wa timu kujituma na kuzingatia nidhamu pindi wanapokuwa uwanjani na nje ya uwanja kwa kuwa kufanya hivyo kutasaidia kila mchezaji kufikia lengo lake la kuwa mchezaji bora.
Kwa upande wa mchezaji wa nafasi ya ushambuliaji (GA) Flora Odilo amewashukuru viongozi wa Wazira pamoja na watumishi wote kwa kuwatia moyo katika michezo amesema wataendelea kushiriki na kucheza kwa bidii ili warudi na ushindi.
Naye mchezaji kwa nafasi ya kiungo mchezeshaji senta (C) Lidya Elisha amesema mchezo ni akili na ushirikiano.