Na Gideon Gregory, Dodoma.
Tanzania imeungana
na mataifa mbalimbali ulimwenguni mwanachama wa umoja wa mataifa kuadhimisha
siku ya mtoto wa kike kimataifa iliyoongozwa na kauli mbiu isemayo “Wakati ni
sasa haki ni Maisha yetu”.
Maadhimisho hayo yamefanyika
leo Oktoba 11,2023 jijini Dodoma katika viwanja vya shule ya sekondari ya
wasichana Msalato na mgeni rasmi alikuwa Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia
Prof. Adolf Mkenda ambapo amesema kuwa idadi ya wasichana waliorejea shuleni kupitia
mfumo rasmi na ambao sio rasmi baada ya kukatisha masomo yao kutokana na
changamoto mbalimbali imeongezeka kwa mwaka 2022/23.
“Idadi ya
wasichana waliorejea shuleni kupitia mfumo rasmi na usio rasmi imeongezeka mpaka
sasa na hadi kufikia 7995 kwa mwaka 2022/23, wanafunzi 676 waliofauru vizuri
kwa masomo ya sayansi wakiwemo wanafunzi wa kike 261 ambapo ni sawa na 41% ya
wanafunzi ambao ya wanafunzi walionufaika na Samia Scoral ship,”amesema Prof. Mkenda.
Aidha Prof. Mkenda
amesema kuwa kulingana na changamoto wanazozipitia watoto wenye mahitaji maalumu
nchini watoe taarifa katika Ofisi ya wizara ya elimu ili waweze kutatuliwa
changamoto na kutimiza ndoto zao.
“Watoto wenye
mahitaji maalumu wenye changamoto ya kusoma watoe taarifa kwatika Ofisi za
wizara ya elimu Sayansi na teknolojia tutajitahidi kuhakikisha kwamba
tunawasaidia kwasababu hayo ni maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan na kazi yetu sisi ni kutekeleza maelekezo yake na
tunayetekeleza kwa raha kwasababu ni maelekezo mazuri mno,”amesema Prof.
Mkenda.
Amesema uwepo wa Mazingira
wezeshi umewezesha watoto wenye mahitaji maalumu kupata elimu na hivyo
kuhakikisha kila mtoto na kila mwananchi anapata elimu hiyo saw ana watu wote
wanavyopata.
Naye mwakilishi wa
Naibu katibu mkuu Elimu Ofisi ya Rais TAMISEMI Bi. Susan Nusu amesema kuwa Ofisi
hiyo inasisitiza kwa hali na mali watu wote kuanzia ngazi ya kaya na mamlaka
zote za serikali Tanzania bara kuhakikisha wanawalinda wototo wote wanakuwa
katika mazingira salama.
“Tunasisitiza kwa
hali na mali viongozi wote kuanzia ngazi ya kaya, mtaa, kijiji, kata wilaya na mamlaka
zote zilizopo katika Mikoa yote ya Tanzania bara kuhakikisha mtoto wa kike si
anarejeshwa shuleni tu lakini anakuwa katika Mazingira salama, anakuwa katika
mikono salama ya watanzania wote wanao mzunguka,”amesema.
Nao baadhi ya wasichana waliorejea shuleni wamempongeza rais Samia kwa kutoa nafasi ya wao kurejea shuleni ili waweze kutimiza ndoto zao na kuwahasa wale walioko shuleni kuhakikisha wanakuwa chachu ya kuwasaidia wenzao wanaopitia changamoto mbalimbali katika jamii.