IDADI YA WACHANGIA DAMU YAONGEZEKA DODOMA.

MUUNGANO   MEDIA
0

 


Na. Gideon Gregory, Dodoma.

Idadi ya wachangiaji damu katika mkoa wa Dodoma imeongezeka kulingana na taarifa iliyotolewa na mhamasishaji wa ukusanyaji damu kutoka katika hospitali ya rufaa mkoa wa Dodoma Dkt. Valeria Elizery.


Dkt. Varelia ameyasema hayo leo Oktoba 30,2023 Jijini Dodoma ofisini kwake wakati akizungumza na Mwandishi wetu kuhusiana na muitikio wa wananchi katika zoezi zima la uchangiaji wadamu.


Aidha ametaja makundi makubwa yenye uhitaji mkubwa wad amu ambapo wanawake wajawazito na ajari a barabarani yamekuwa makundi ambayo yanatumia zaidi damu kila mwaka.


Sanjari na hayo ameshauri watu wengine kuendelea kujitokeza kuchangia damu kwani damu haiuzwi sehemu yoyote kama madawa na dripu.


Nao baadhi ya wachangiaji wamezungumza baada ya kuchangia ambapo wamesema kuwa suala la kuchangia damu halina shida yoyote kama watu wanavyosema mitaani na kuwaomba kuendelea kujitokeza kwa wingi kuweza kuwasaidia wahitaji.

Tags

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)