Spika wa Bunge la Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) kwa Kundi la Afrika Mhe. Dkt. Tulia Ackson, leo tarehe 21 Oktoba, 2023 ameongoza kikao cha Maspika wa Kanda ya Afrika kuhusu ajenda zitakazojadiliwa katika Mkutano Mkuu wa 147 wa IPU unaotarajiwa kufunguliwa rasmi tarehe 23 Oktoba, 2023 Jijini Luanda, Angola.

.jpg)

