DAC MTWARA AFUNGUA MAFUNZO YA UTEKELEZAJI WA MFUMO WA ANWANI ZA MAKAZI.

MUUNGANO   MEDIA
0

Na. Simon Kibarabara Mtwara.

Katibu Tawala wa Wilaya ya Masasi Mkoa wa Mtwara Bi.Fatma Said Kubenea, leo Oktoba 06, 2023 amefungua mafunzo ya siku Mbili ya Utekelezaji wa Mfumo wa Anwani za Makazi kwa Wenyeviti wa Serikali za Mitaa,  Watendaji wa Kata na Mitaa pamoja na wakusanya Taarifa wa Halmashauri  ya Mji wa Masasi.


 Akifungua mafunzo hayo yaliyofanyika katika Ukumbi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Masasi. Katibu Tawala ametumia nafasi hiyo kuwataka Wenyeviti na Watendaji wa Mitaa kushirikiana na wajumbe wa Serikali za Mitaa pamoja na wananchi kwa ujumla ili kuhakikisha kazi ya kuhakiki taarifa za Anwani za Makazi inafanikiwa na kuleta tija iliyokusudiwa. 


“Anwani ya Makazi ni hitaji la msingi katika kuwezesha ukuaji wa Sekta mbalimbali za kijamii na kiuchumi na ni Nyenzo muhimu ya ukuaji wa Uchumi wa kidijitali ambao ndio umeshika Kasi.

Tags

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)