CHONGOLO ARIDHISHWA NA UTEKELEZAJI MIRADI HALMASHAURI YA MLELE.

MUUNGANO   MEDIA
0

 

Baadhi ya wanachama wa chama Cha Mapindunzi CCM halmashauri ya Mlele wakiwa na Katibu Mkuu CCM Daniel Chongolo kwenye eneo la mradi.


Eneo la kituo cha kupozea umeme Inyonga kilichokaguliwa na Katibu wa CCM Daniel Chongolo.

Na. Mary Baiskeli, Katavi.

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapindunzi CCM Daniel Chongolo ameridhishwa na utekelezaji wa miradi katika halmashauri ya wilaya ya Mlele akidai kuwa wameitendea haki Ilani ya chama kwa kukidhi Vigezo.

Chongolo akiwa mkoani Katavi amedhuru halmashauri ya wilaya ya Mlele Oktoba 5,2023 Kisha kukagua bwawa la Senkwa ambalo linajengwa ili kuwahudumia Wakazi zaidi 68,000 kutoka vijiji 16.

Amesema endapo kuna wananchi wanaishi ndani ya chanzo hicho cha maji wanatakiwa kupisha ili kukilinda kwakuwa kina manufaa makubwa kwa jamii.

Mbali na kukagua mradi huo ametembelea shule ya Sekondari Inyonga pamoja na kituo cha kupozea umeme Inyonga akiridhishwa na Maendeleo yake.

Pia amekagua barabara na kubaini hatua kubwa iliyofanyika ikiwamo barabara nyingi za mitaa zimejengwa kwa lami tofauti na maeneo mengine.

Baada ya kukagua miradi hiyo amezungumza na Wakazi wa Inyonga ikalazimu kutoa pongezi hizo Mbele ya halaiki akieleza namna usimamizi wa miradi ulivyo tukuka na kwamba halmashauri zingine zinatakiwa kuiga mfano huo.

"Mlele mpo vizuri sana sina cha kusema nakupongeza Mkuu wa wilaya, Mkurugenzi na watumishi wote mnachapa kazi,wananchi wanaona hakuna wa kuwalaghai,"

"Changamoto ya mgogoro wa ardhi mpaka kuingia hifadhini nitalifikisha kwa rais suala hili litafutiwe ufumbuzi," amesema Chongolo akaongeza.

Pia amesema kuhusu maombi yaliyotolewa na Mbunge wa Jimbo la Katavi Izack Kamwelwe kuhusu uhitaji wa kujengewa chuo Cha afya katika eneo la Inyonga ameahidi kushughulikia mapema iwezekanavyo.

"Mimi ni mshauri wa rais nitamweleza suala hili ni muhimu endeleeni kutenga eneo mapema la kujenga chuo watu wanaopenda Maendeleo na wanasimamia vizuri lazima wapewe fursa," amesema Kamwelwe.

Aidha amesisitiza suala la kuongeza uzalishaji wa mazao kwakuwa Katavi ni kitovu Cha kilimo Cha biashara na chakula.

Awali Mbunge wa Jimbo la Katavi Izack Kamwelwe akituma salamu zake kwa rais amemuomba Katibu Mkuu CCM kumfikishia maombi hayo ya kujengewa chuo Cha afya kitachoongeza idadi ya watumishi.

"Vituo vya afya, zahanati na hospitali vipo tunahitaji kupata chuo Cha afya ili watalaam waongezeke tuombee kwa rais,"amesema Kamwelwe.

Naye Mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko ameeleza hatua madhubuti zinazochukuliwa na mkoa ni kuimarisha usimamizi wa miradi na shughuli za kiutendaji.

"Tunamshukru rais ametuletea miradi mingi Sana hatuna Cha kumlipa tunaendelea kuisimamia,"amesema Mrindoko.

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)