Timu ya Wanawake ya Mpira wa Pete ya Haki Sports Club jioni ya leo imeng'ara tena baada ya kujinyakulia ushindi na pointi tatu muhimu dhidi ya timu ya RAS Iringa.
Akizungumza mara baada ya mchezo huo Kaptein wa timu hiyo ya Haki Bi. Catherine Saoke amesema kuwa, ushindi huo umepatikana kutokana na kuwa na maandalizi mazuri ya mashindano hayo.
Aidha timu hiyo imeendelea kujiweka sawa kwa ajili ya mchezo wa kesho ambapo kwa upande wa kamba itamenyana na Mawasiliano na upande mpira wa pete itamenyana na MSD.
Kwa upande wa wanaume kesho mapema asubuhi timu ya Haki itamenyana na TARURA.