SERIKALI KUENDELEZA MAPAMBANO DHIDI YA MAGONJWA YA UKIMWI NA KIFUA KIKUU.

MUUNGANO   MEDIA
0

 


OR-TAMISEMI.

Serikali imesema itaendelea kuwekeza rasilimali fedha na watu kwenye mapambano dhidi ya magonjwa ya UKIMWI na kifua kikuu ili kuzuia maambukizi mapya ifikapo mwaka 2030.


Hayo yamesemwa na Naibu Katibu mkuu Ofisi ya Rais-TAMISEMI anayeshugulikia Afya Dkt. Wilson Mahera wakati wa ufunguzi wa kikao cha tathmini ya mapambano dhidi ya magonjwa ya UKIMWI na Kifua kikuu kilichohusisha Waganga Wakuu wa Mikoa na Wilaya kilichofanyika jijini Dodoma 


“ Malengo ya Serikali ni kuzuia kabisa maambukizi mapya ya VVU na kutokomeza ugonjwa wa kifua kikuu ifikapo mwaka 2030, kwa kushirikiana na wadau kama mfuko wa Dunia na wengine  hivyo tunaamini tutatimiza hilo, ' amesema Mahera


Amesema Serikali imewekeza  kwenye ujenzi wa miundombinu ya ujenzi na vifaa tiba  ambapo mkakati wa sasa  ni  utoaji wa huduma bora za afya ili kupunguza,kuzuia na kumaliza kabisa magonjwa hayo.

Dkt Mahera amewagiza  washiriki wa tathmini hiyo waboreshe mpango kazi wa mapambano uliopo ili uendane na wakati wa sasa.


Vilevile, ,Dkt.Mahera ametumia kikao hicho kuwakumbusha  Waganga Wakuu wa  Mikoa na  Wilaya kuhakikisha  vituo vyote vya kutolea huduma za afya  vilivyokamilika vinasajiliwa na kuanza kutoa huduma kwa wananchi.


"Itakuwa jambo la ajabu viongozi watakapoanza ziara na kukuta vituo vya kutolea huduma za afya  havijaanza kutumika kwa sababu vimechelewa kusajiliwa kwa uzembe wa mtu, serikali ya awamu ya sita imewekeza fedha nyingi sana  kwa kujenga vituo hivi pamoja na kununua vifaa tiba vya kisasa , ni wakati wa wananchi kufurahia hizo huduma bora"  ameagiza Dkt, Mahera.






Tags

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)