Na Beatus Maganja.
Kundi la watalii wa ndani wapatao 21 Julai 6, 2023 wametumia kikamilifu ofa maalum ya Sabasaba kwenda kutalii katika Hifadhi ya Magofu ya kale Kilwa Kisiwani iliyo chini ya Usimamizi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA).
Ofa hii imelenga kuhamasisha Utalii wa ndani na kuwawezesha watanzania wote kutembelea hifadhi hiyo Kwa kupunguzo kubwa la gharama ambapo mtalii Kwa kulipia gharama ya Shillingi 130,000/= ataweza kutalii baharini katika visiwa vya Kilwa Kisiwani na Songo Mnara Kwa kutumia boti la Kisasa lenye kioo maalum chenye kumwezesha mtalii kuona mandhari na viumbe mbalimbali vilivyopo chini ya bahari Kwa siku mbili
Kupitia malipo ya kiasi hicho mtalii pia ataweza kupata chakula, vinywaji na viburudisho mbalimbali
Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) inaendelea kuwahamasisha watanzania wote kutumia kipindi hiki cha maonesho ya Sabasaba kutembelea hifadhi zake zote nchini hususan Kilwa Kisiwani na Songo Mnara kwani ni kipindi maalum chenye punguzo maalum Kwa watalii wa ndani.