Na.Elimu ya Afya kwa Umma.
Mpendwa msomaji wa safu hii ikiwa tukiwa katika mwezi
huu Julai 14.2023 wa mtindo wa Maisha katika afya(Monthly
Healthy Life Styles) Elimu ya Afya
kwa Umma inatumia fursa hii kukukumbusha
kufanya na kuzingatia yafuatayo ili kuendelea kuimarisha afya yako kwani Mtu ni
Afya.
Tumia muda wako kutembea kuliko kuendesha
gari(Walk more ,Drive less)
Mara kwa mara
ili kuimarisha afya yako zaidi unashauriwa kutumia muda wako mwingi
kutembea kuliko kutumia vyombo vya usafiri kama vile magari, pikipiki,bajaji na
vinginevyo vingi kwani hii itasaidia mwili wako kuwa imara na kuepukana na
magonjwa yasiyo ya kuambukiza ,unene kupita kiasi na msukumo wa damu utafanya
kazi vizuri, pia utaepuka magonjwa ya moyo na shinikizo la juu la damu.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Dkt.Philip Mpango katikati akiongoza katika mazoezi ya kutembea
moja ya tukio muhimu la bonanza,upande wa kushoto ni Waziri Mkuu Kassim
Majaliwa na upande wa kulia ni Spika wabunge Dkt.Tulia Ackson .
Rais Mstaafu awamu ya nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiongoza wapanda mlima Kilimanjaro pamoja na Waendesha baiskeli wanaoshiriki katika kampeni ya kuchangia fedha za afua ya masuala ya UKIMWI.
Ongeza ulaji wa mbogamboga na matunda katika mlo wako(Increase
Vegetables and Fruits in your diet).
Mtindo huu wa ulaji wa mbogamboga na matunda unasaidia
mwili kupata virutubisho muhimu katika mwili ikiwemo Vitamin C, B6 na K Fat na
madini ya shaba na manganese ,kupunguza uwezekano wa magonjwa ya saratani
,Kisukari na maradhi ya moyo ,kuondoa sumu mwilini na kuondoa msongo wa mawazo
,usaidia kupona haraka ukifanyiwa upasuaji hasa ulaji wa tunda la nanasi na
matunda mengine mengi.
Baadhi ya matunda ambayo ni muhimu kwa ajili ya kujenga afya ya miili yetu.
Punguza ulaji wa vyakula vyenye mafuta na lehemu(Reduce Fats and Cholesterol in your diet ).
Tunaposema lehemu ni
mafuta yanayoongezwa mwilini kupitia chakula ,mfano unapokula nyama yale mafuta
ya nyama ambayo yana uwezo mkubwa wa kuganda yanaitwa lehemu.
Ikumbukwe kuwa kuna aina mbili za lehemu ambazo ni
lehemu nzuri(good cholesterol) na
lehemu mbaya(bad cholesterol),hivyo uwepo wa lehemu mbaya mwilini ndio
chanzo kikuu cha uharibifu wa mishipa ni
muhimu kupunguza mtindo wa ulaji wa nyama zenye mafuta mengi hasa nyekundu ili
kuepuka magonjwa yasiyoambukiza.
Kunywa maji kwa wingi (Drink more Water).
Kiafya binadamu anashauriwa kunywa maji kwa wingi
kwani maji yana faida nyingi ikiwemo kusaidia kuboresha afya ya mfumo wa mkojo
hivyo kunywa maji ya kutosha kunasaidia kuondoa hatari ya magonjwa ya Kibofu
cha mkojo,maji husaidia kudumisha uzito, kurahisisha mmeng’enyo wa chakula na
kuzuia kuvimbiwa,pia maji yana faida kubwa ya kudumisha kumbukumbu na tafiti
zinabainisha kuwa mtu akipungukiwa na maji kidogo tu hupoteza kumbukumbu kwa
rika lote mtoto au mzee.
Unywaji wa maji ya kutosha ni muhimu katika miili yetu.
Punguza
muda wa kutazama runinga na matumizi ya
kompyuta muda mrefu(Reduce your Screen time(TV and Computer).
Katika ulimwengu huu wa utandawazi matumizi ya runinga na kompyuta yameongezeka
maradufu hali ambayo imechagiza watu wengi kutumia muda mwingi kutumia vifaa
hivyo vya kielektroniki iwe ofisini au nyumbani licha ya faida yake kuna
madhara kiafya mfano kuchosha akili na kukosa muda wa kufikiri.
Fanya
Mazoezi ya mwili Mara kwa Mara(Exercise
more (body and mind).
Katika mtindo huu wa kufanya mazoezi mara kwa mara
inasaidia mwili kuwa imara kwani mtu anayefanya mazoezi anakuwa na akili inayofikiri na
kuchanganua mambo kwa uharaka zaidi, pia mwili wake utakuwa imara katika
kukabiliana na magonjwa kama vile maradhi ya moyo .
Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akiongoza zoezi la
kufanya mazezi ya mwili mojawapo ya bonanza la afya hapa nchini.
Waziri wa Afya Mhe.Ummy Mwalimu akishiriki
mazoezi ya viungo na baadhi ya watoto wenye mahitaji maalum katika kuimarisha
afya ya mwili.
Kula vyakula tofauti tofauti na vyenye virutubisho vyote muhimu mwilini (Eat
a Variety nutritional of Foods).
Ni muhimu kula vyakula tofauti tofauti na vyenye
virutubisho vyote katika mwili kwa kuzingatia makundi yote ikiwemo
Protini,Vitamin,Hamirojo kwani hali hiii itasaidia kuujenga vizuri mwili na
itakuwa kinga dhidi ya magonjwa .
Kwa hiyo kupitia mambo yote hayo itatusaidia kuijenga
miili yetu kuwa na afya njema na kuweza
kutekeleza majukumu katika ujenzi wa taifa na kila mmoja ana jukumu la kujenga
Afya yake kwani ukiwa na afya
dhaifu huwezi kufanya chochote na jukumu
la Elimu ya Afya kwa Umma ni kuelimisha
hivyo sote tujumuike ili kutimiza
adhma ya Serikali ya awamu ya Sita chini ya Rais Mpendwa Dkt.Samia Suluhu
Hassan pamoja na Waziri wa Afya Mhe.Ummy
Mwalimu ambapo moja ya vipaumbele ni kuhakikisha afya msingi inakuwa bora kwa
kila jamii.
MWISHO.