KAMPUNI YA NKONYA INVESTMENT YAKARIBISHA WADAU WA MADINI KUTUMIA BIDHAA ZAKE BORA.

MUUNGANO   MEDIA
0

Kampuni ya Nkonya Investment inayojihusisha na usambazaji wa vifaa vya usalama kazini imekaribisha wadau wa madini nchini ikiwa ni pamoja na kampuni za uchimbaji wa madini, watafiti wa madini na ujenzi nchini kutumia bidhaa bora wanazozalisha badala ya kuagiza kutoka nje ya nchi.


Akizungumza kwenye mahojiano maalum, Mkurugenzi wa Kampuni ya Nkonya Investment, Dkt. Daniel Nkonya, leo Julai 07, 2023 kwenye kilele cha Maonesho ya Kimataifa ya Sabasaba yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, amesema kuwa kampuni yake iliyoanza tangu mwaka 2016 imekuwa na rekodi ya kuzalisha bidhaa zenye ubora wa hali ya juu ikiwa ni pamoja na sare za migodini, helmets, viatu, gloves, gas detectors, na vifaa vingine vya kujilinda kwenye shughuli za uchimbaji wa madini (PPEs).


Amesema kuwa, kampuni imekuwa na uzoefu mkubwa wa kutoa huduma katika migodi mikubwa ikiwa ni pamoja na Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGML), Mgodi wa Dhahabu wa Shanta, Mgodi wa Almasi wa Mwadui, Mgodi wa Dhahabu wa Barrick na migodi mingine midogo

Aidha, ameongeza kuwa kampuni imekuwa ni msambazaji mkubwa wa bidhaa kwenye migodi inayomilikiwa na Serikali ikiwa ni pamoja Mgodi wa STAMIGOLD unaomilikiwa na Shirika la Madini la Taifa (STAMICO).


Akizungumzia huduma zinavyotolewa na kampuni yake, Dkt. Nkonya amefafanua kuwa huduma zinapatikana nchi nzima kupitia ofisi zake zilizopo katika maeneo ya Kunduchi, Dar Salaam; Isamilo jijini Mwanza; na mtaa wa Bomani mjini Geita.


Ameongeza kuwa ili kuhakikisha bidhaa zinamfikia kila mteja, ofisi ina utaratibu wa kusafirisha bidhaa mpaka mahali mteja alipo popote nchini.


Akielezea mipango ya kampuni yake kwenye uboreshaji wa huduma, Dkt. Nkonya amesisitiza kuwa kampuni ina mpango wa kufungua ofisi katika mikoa yote nchini pamoja na nchi za jirani za Afrika Mashariki na Kati.



Ameendelea kusema kuwa wanapatikana kwa mawasiliano ya namba za simu 0715767675 na email info@nkonya.co.tz

Tags

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)