Halawa
Lubana ni mkulima na mkazi wa Kijiji cha
Ikulwe Kata ya Majimoto Halmashauri ya
Mpimbwe Wilayani Mpanda Mkoani Katavi mwenye familia ya watu 26 na mwaka
huu amevuna magunia 525 badala ya 700
aliyozoea huku mahitaji ya familia kwa mwaka ni ulaji wa magunia
108 ambapo ametumia fursa hiyo kuwaasa
Vijana kuacha kukimbilia mjini bila kazi bali wajikite katika kilimo.
Akizungumza Kijijini
hapo Halawa amesema kwa siku familia yake hula debe mbili na mwezi gunia sita
hivyo bila jitihada za kulima angeukimbia mji.
“Nawasihi wanaokimbilia
mjini bila kazi yoyote waache kwani
ukikimbilia huko mwisho wa siku unakuwa kibaka waje vijijini tulime ,kwa siku
natumia debe 2 kwa mwaka magunia 108 bila kukaza buti ningeukimbia mji na mwaka huu hali siyo nzuri nimepata magunia 525
ya mpunga na mwaka ukiwa mzuri navuna zaidi ya magunia 700”amesema Lubana.
Katika hatua
nyingine Lubana ametoa ushauri kwa serikali kuwasaidia wakulima kupata fursa ya
kupima wao wenyenye pindi wanapouza mazao kuliko kupimiwa na wafanyabiashara
kwa kutumia ndoo kubwa{rumbesa) huku akitoa shukurani soko la Mpunga kuendelea
kuimarika siku hadi siku kwani sasa gunia moja la mpunga wilaya ya Mpanda
linauzwa zaidi ya Tsh.laki moja.
TAZAMA VIDEO HAPA CHINI